Saturday, February 11, 2017

WAPINZANI WA ZIMAMOTO KATIKA MICHUANO YA CAF WAWASILI ZANZIBAR


zimamoto
WAPINZANI wa Zimamoto kwenye michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Ferroviario de Beira imeshawasili Zanzibar katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikitokea Msumbiji na wapo tayari kwa ajili ya pambano litakalo pigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Amaan Saa10:00 za jioni.
Timu hiyo ya Ferroviario de Beira ambao ni mabingwa wa ligi kuu soka ya Msumbiji, wamefikia katika Hoteli ya Mtoni Marine iliopo Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ambapo msafara wao umekuja na wachezaji 20 pamoja viongozi 7.
Kikosi hicho ambacho kina wachezaji watano wa kigeni kilipokelewa na viongozi wa ZFA akiwemo Makamo wa rais, Katibu mkuu na Afisa habari wa chama hicho sambamba na viongozi wa Zimamoto.
Miongoni mwa wachezaji wageni ni pamoja na Fabrice Sikanda kutoka Congo ambaye amesema wanaifahamu kiasi Zimamoto na ni timu ambayo kamwe haiwezi kuwapa shida.
“Sisi tumekuja hapa Zanzibar kuchukua point na kurudi nyumbani, Zimamoto tumeshaiona katika Kombe la Mapinduzi kwenye TV, hivyo kichapo wanacho tu mana wanafungika vizuri tu”. Alisema Sikanda.

No comments :

Post a Comment