Saturday, February 11, 2017

RC IRINGA AINGIA DARASANI KUFUNDISHA , AAGIZA WILAYA YA MUFINDI KUINGIA 10 BORA UFAULU KITAIFA


DARASANI
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa mwalimu  Amina Masenza akifundi somo  la Uraia kwa  wanafunzi wa  kidato  cha tano  shule ya  sekondari  Sadani  wilaya ya  Mufindi leo baada ya  kufanya  ziara  shuleni hapo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza  akifundisha somo la urai
Mkuu  wa mkoa wa  Iringa mwalimu Amina Masenza akipokelewa  shule ya sekondari Sadani
Mkuu  wa  wilaya ya   Mufindi Wiliam Jamhuri akimkaribisha  mkuu wa mkoa wa Iringa
Watalam  wa  mkoa wa Iringa
Walimu na viongozi wa wilaya ya  Mufindi
Watumishi  wakimsikiliza  mkuu wa mkoa
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Sadani Mufindi Yusuph Mwagala
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Sadani Mufindi Yusuph Mwagala akipongezwa na mkuu wa  mkoa  wa Iringa Mwalimu Amina Masenza
Mkuu wa mkoa  wa Iringa mwalimu Amina Masenza na mkuu wa  wilaya ya  Mufindi Wiliam Jamhuri  wakifungua daharia  ya  wasichana  shule ya  sekondari Sadani
Rc  akikagua  daharia  hiyo
Bwalo la chakula  Sadani  Sekondari  ambalo linahitaji wadau  kuchangia ili kukamilika
Rc Mwalimu Masenza  akitoka kukagua  bwalo  hilo
Mwanafunzi wa kidato cha  sitta  Sadani  sekondari Sagendo Fadhili  akijibu maswali ya  mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu  Amina Masenza
Mkuu  wa mkoa wa Iringa  Mwalimu Amina Masenza  akiendelea  kufundisha  wanafunzi wa  kidato cha nne   shule ya  sekondari  sadani
Mkuu  wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza akiwa na mkuu wa shule ya Sadani katikati na mkuu wa wilaya ya Mufindi Bw Wiliam Jamhuri  kushoto
Walimu  wa  Sadani Sekondari  wakifurahia  ziara ya mkuu wa mkoa shuleni hapo na kuomba kusaidiwa  kusogezewa  umeme wa  Rea  shuleni hapo
Mwalimu Masenza mkuu wa mkoa  wa Iringa  akiteta na  walimu wenzake wa  shule ya  sekondari Sadani Mufindi
Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Mwalimu Amina Masenza (wa nne kushoto)  akiwa katika  picha ya pamoja na walimu wa  shule ya  sekondari  Sadani


Na  MatukiodaimaBlog
MKUU  wa  mkoa wa
Iringa Amina Masenza amelazimika  kuingia darasani kufundisha kama njia ya kuwataka walimu kuwajibika kufundisha  huku akiuagiza
uongozi wa  wilaya  ya Mufindi kuhakikisha wanaweka mikakati
itakayoiwezesha  shule ya sekondari ya
Sadani kuingia katika nafasi  ya 10 bora
katika mitihani ya kitaifa mwakani  2018.
Huku akichangia
kiasi  cha Tsh milioni 1 kwa ajili
ya ujenzi wa bweni la  wanafunzi  shuleni hapo
kama sehemu ya maandalizi ya shule
hiyo kujiandaa kuwa shulebora kitaifa.
Mkuu  huyo  wa mkoa ametoa agizo hilo  leo wakati wa ziara  yake ya
ukaguzi na ufunguzi wa  bweni la
wanafunzi wa  kike  katika
shule  hiyo,kuwa kutokana na
mkoa  wa
Iringa  kufanya vema  katika
mitihani ya Kitaifa ya
kidato  cha  nne kwa
kuwa mkoa wa pili kitaifa ila bado wilaya ya Mufindi  inapaswa kuhakikisha shule  hiyo
kuwa  kati ya shule  10 bora kitaifa .
Alisema  kuwa  moja katika ya maagizo ambayo anataka
mkurugenzi  wa Halmashauri ya  wilaya ya Mufindi kufanya ni kuandaa
mkataba  maalum, kati ya  waslimu
wa shule  hiyo ya mkurugenzi
mkataba ambao atausaini kwa  ajili ya
ofisi yake na mkuu wa wilaya ya Mufindi kuingia mkataba iwapo watashindwa  kuingia katika  shule 10 bora basi watamtafuta aliyekwamisha
mkataba illi achukuliwe hatua.
“ Mkataba  hii itakuwa
kwa  walimu wote  wa mkoa wa Iringa ili kupima uwezo wa  walimu katika kutimiza wajibu  waokatika utendaji kazi  ili kama mwalimu asiyewajibika basi  kukaa pembeni ili kupisha mwalimu ambae
anafanya kazi  kwa ari ya  kujituma zaidi”
Hata hivyo aliwataka
walimu kufanya kazi  kwa  kutimiza
wajibu wao     badala ya  kufanya kazi
kwa  mazoea kwa  kukimbilia
kudai haki  zao badala  ya kufuata
taratibu.
Alisema  wapo  baadhi ya
walimu  wanalalamika kudai
haki  zao
ila wamekuwa wakiendea  kutibiwa
nje ya  mkoa  bila
hata ya  kufuata taratibu za
kuandika barua na  kuwataka  kuzingatia
taratibu  za  kazi kwa kutunza  kumbukumbu
mbali mbali katika mafaili  yao.
Kuhusu ujenzi  bweni
na umaliziaji  wa bwalo la chakula  shuleni hapo
aliagiza  mkuu  wa
wilaya  kuitisha kikao  na wafanyabiashara   ili
kusaidia ujenzi huo na shughuli za
kimaendeleo shuleni hapo.
Pia  alipongeza
jitihada  kubwa  zinazofanywa na uongozi  wa  shule  hiyo
chini  ya mkuu wake Yusuph Mwagala
kutokana  na kuendelea  kufanya shule
hiyo  kuwa mbeli  kielimu pamoja na  maendeleo mengine
Awali mkuu  wa  shule
hiyo Bw Mwagala  alisema  kuwa
shule  hiyo  imeendelea
kufanya  vema  katika nafasi ya  kimkoa na
kitaifa  ambapo   mwaka
2015 katika  matokeo  ya kidato
cha nne ilishika  nafasi  ya 64 kati ya shule 131 kimkoa na kiwilaya
ilishika nafasi ya 26 kati ya shule  54
wakati kwa mwaka  huu imeshika nafasiya
25 kati ya  shule 152 kimkoa na nafasi ya
8 kati ya 42 kiwilaya
Pia  alisema  mbali ya mafanikio katika  elimu
bado  shule  hiyo inakabilia na changamoto mbali mbali
kamaupungufu  wa mabweni  ya
wanafunzi wa kidato cha tano na
sita upungufu ambao  unatokana
na  ongezeko  kubwa
la  udahiri  wa
wanafunzi wa  kidato cha tano
kulingana  na  miundo mbinu iliyopo kabla ya  kuanzisha kidato  cha tano na
sita ,upungufu  na uchakavu wa
vyumba  vya  madarasa,ukosefu  wa
umeme ,ukosefu  wa bwalo  la
chakula, upungufu wa  walimu  8 wa masomo ya sayansi  ,walimu watatu  wa somo la biolojia, walimu   wawili
wa masomo ya fizikia ,walimu
watatu  wa kemia  na
hesabu  mwalimu mmoja ,ukosefu
wa  maabara ya  biolojia.
MWISHO

No comments :

Post a Comment