Bingwa wa dhahabu kwenye mashindano ya London 2012, Mariya Savinova wa Urusi, avuliwa taji lake
Mshindi wa nishani ya dhahabu
mwaka 2012 katika mbio za mita 800 za huko London Mariya Savinova,
amevulia taji lake na kupigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya
mbio hadi mwaka 2019.
Matokeo yote ya mbio za
mwanariadha huyo tangu Julai 10, 2010 hadi Agosti 2013, zimefutiliwa
mbali, baada ya kupatikana ametubia dawa za kusisimua misuli.
Savinova alimpiku Caster Semenya
wa Afrika Kusini katika mashindano hayo ya Olimpiki Jijini London na pia
mbio za dunia za riadha mwaka 2011 huko Daegu, Korea Kusini.
Mkimbiaji huyo mwenye umri wa
miaka 31 pia alimshinda Muingereza Jenny Meadows katika mbio za mataifa
ya Bara Ulaya mwaka 2010 na kumfanya kunyakua medali ya shaba. Sasa
medali zote za wanariadha hao wawili Jenny Meadows na Caster Semenya
zitaboreshwa.
Savinova pia atapoteza dhahabu
yake katika mbio za mita 800 ya mwaka 2011 pale aliposhinda mashindano
ya mataifa bingwa barani Ulaya.
Taarifa kutoka katika mahakama
inayosikiza makosa ya kimichezo: “Kwa misingi ya ushahidi tosha,
ikijumuisha pia ushahidi kutoka kwa hati ya kuzaliwa (ABP), Mariya
Savinova amepatikana akijihusisha na utumiaji wa dawa za kusisimua
misuli tangu Julai 26, 2010 (Usiku wa kuamkia mashindano ya mataifa
bingwa Ulaya yaliyokuwa yakifanyikia mji wa Barcelona) muda wote hadi
Agosti 19, 2013 (siku ya mashindano ya dunia Jijini Moscow).
Savinova ni miongoni mwa
wanariadha watano wa Urusi waliotajwa katika ripoti ya na mamlaka kuu ya
kukabiliana na dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha (WADA).
Hajashiriki mbio tangu mwaka 2013
pale aliposimamishwa ili achunguzwe baada ya video kuhusu matumizi ya
madawa hayo kufichuliwa na mpekuzi Yuliya Stepanova.
No comments :
Post a Comment