Saturday, February 11, 2017

WADAU WATAKIWA KUENDELEZA NA KUDUMISHA UTAMADUNI


WAU1
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (katikati) akishirikiana na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu kukata utepe kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam
WAU2
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (kushoto) akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la Bodi ya Filamu Tanzania wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
WAU3
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (wapili kushoto) akiangalia moja ya kitabu kilichofanyiwa marekebisho na wataalamu kutoka Iran baada ya kuchakaa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BASATA Bw. Godfrey Mngereza
WAU4
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (Wanne kulia) akiangalia bidhaa za kiutamaduni za Iran zinazotengenezwa na malighafi za shaba, fedha na dhaabu kutoka kwa Bw. Anmad Hamidi (kulia) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi
WAU5
Kikundi cha kiutamaduni kutoka Iran kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
WAU6
Kikundi cha ngoma kiitwacho Jivunie Tanzania Sanaa Group kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
WAU7
Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam
WAU8
Watoto wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran wakiimba wimbo wa taifa wa Iran wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
WAU9
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (katikati) akifuatilia maonyesho yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi na kulia ni Mkurugnzi Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achiles Bufure
WAU10
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (kulia) akizungumza na watu walioshiriki katika maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
WAU12
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (kushoto mwenye sahani) akiongoza watu walioshiriki katika maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni kuonja chakula cha watu wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran  leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi
…………………………………………………………………………………..
NA Genofeva Matemu.
Wadau wa utamaduni nchini wametakiwa kutumia maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi kuenzi, kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa kiutamaduni katika tasnia ya Lugha, Sanaa, Filamu, Mila na Desturi za Tanzania na Iran.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni.
“Uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Iran ulianza tangu karne ya 18 kipindi cha majilio ya wahenga wa kishirazi kutoka uajemi ulioacha turathi za kiutamaduni za pande zote mbili” amesema Bw. Ryatuu.
Aidha, Bw. Ryatuu ameushukuru uongozi na watumishi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni katika kufanikisha sherehe hii adhimu ya wiki ya utamaduni wa Washirazi.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi ameushukuru uongozi wa Tanzania kuendeleza na kuthamini utamaduni wa washirazi unaounganisha nchi ya Iran na Tanzania.
Washirazi walikuja nchini tangu karne ya 18 kufanya biashara katika Pwani ya Bahari ya Hindi na mji wao wa kwanza kufika ulikua ni Kilwa mji ambao uliweza kustawi kiuchumi na kuweza kujitengenezea fedha zake yenyewe na kufanya biashara na miji yote ya Pwani ya Afrika Mashariki.

No comments :

Post a Comment