Kamishna wa Makao Makuu wa
Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Rosaldina Majuva alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya chama hicho
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es
Salaam, kutoka kulia Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa Hangi na
Katibu wa chama hicho, Grace Shaba.
Katibu wa chama cha Tanzania Girl
Guides Association (TGGA), Grace Shaba akifafanua kuhusu malengo ya
chama hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa
Hangi, kushoto ni Kamishna wa Makao Makuu wa chama hicho, Rosaldina
Majuva.
…………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Tanzania Girl Guides Association
(TGGA) wanategemea kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa njia
ya kufanya shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii.
Maadhimisho hayo yanayojulikana
kama ‘thinking day’ yatafanyika Februari 22 mwaka huu ambapo shughuli za
kuisaidia jamii zitaanza Februari 10 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Kamishna wa Makao Makuu wa Chama hicho, Rosaldina Majuva
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.
Bi. Rosaldina amesema kuwa siku
ya maadhimisho ya chama hicho inaambatana na siku ya kumbukumbu ya
kuzaliwa kwa waasisi wao akiwemo Lord Baden Powell ambaye alikuwa
kiongozi wa Boy Scout pamoja na Kamishna Mkuu wa Girl Guides na Girl
Scouts, Lady Olave Baden Powell (mkewe).
“Tumepanga kuadhimisha siku hii
muhimu kwa kufanya shughuli za kijamii zikiwemo za kutoa misaada kwa
wahitaji, kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach
na Magomeni na kupanda miti, kutoa elimu ya kujithamini, kujitambua na
kukataza unyanyasaji pamoja na kutembelea kituo cha wazee wa
Kigamboni,”alisema Bi. Rosaldina.
Kwa upande wake Katibu wa chama
hicho, Grace Shaba amefafanua kuwa chama hicho kimelenga kupanua uelewa
wa wanawake kwa ujumla kuhusu uzalendo, majukumu ya nchi yao, kujenga
ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia kambi za mafunzo, kutembelea
na kuwasiliana kwa njia za teknohama pamoja na kuwa tayari kufanya kazi
kwa manufaa yao na ya Taifa.
“Dira yetu ni kuwa na jamii yenye
wasichana na wanawake waliowezeshwa kufikia uwezo wa juu kabisa katika
kutimiza malengo yao na kuwa rasilimali bora ya Taifa,”alisema Bi.
Grace.
Nae Kamishna Mkuu wa Tanzania
Girl Guides Association, Symphorosa Hangi amesisitiza wanawake na watoto
wa kike kujiunga na chama hicho kwani kinatoa elimu ya masuala ya
kijamii na kiuchumi yatakayosaidia kuwainua wanawake na watoto pamoja na
taifa kwa ujumla.
Mpaka sasa kwa Tanzania,chama hicho kipo katika mikoa 22 kikiwa na jumla ya wanachama
No comments :
Post a Comment