Baadhi ya watumishi kutoka Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kampuni ya Udalali ya Msolopa
Investment na baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Ofisi ya
Mohammed Enterprises iliyopo jingo la Golden Jubilee mara baada ya
wafanyakazi wa Mohammed Enterprises kukimbia.
Wafanyakazi wa Lamada Hotel
(kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati
ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.
Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya
Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya
Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya
kodi ya ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na
waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu
au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya
serikali.
……………
Wizaraya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya
Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya
kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.
Katika hatua ya kwanza Wizara kwa
kushirikiana na Manispaa za za mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa
wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises
anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada Hotel anaedaiwa Shilingi milioni
54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)
anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi
milioni 22
Makampuni hayo yamepewa notisi ya
siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa
umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.
Serikali kwa kutumia kampuni ya
Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika
katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo
mbalimbali nchini.
Akiongea kwa kusisitiza, Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga
kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.
Wizara haitaweza kufanikisha
malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki
kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali
yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi
ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.
No comments :
Post a Comment