Waandishi wa habari wakiwa kazini
wakati wa mkutano wa Gavana wa Jimbo la Haut Katanga Bw. Jean – Claude
Kazembe Musonda (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakiwa kazini
wakati wa mkutano wa Gavana wa Jimbo la Haut Katanga Bw. Jean – Claude
Kazembe Musonda (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Gavana wa Jimbo la Katanga katika
Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) Jean Claude Kazembe ametoa wito kwa
wananchi na wafanyabiashara kutoka nchini DRC kutumia
Bandari ya Dar es
Salaam kwa kuwa imeimarisha utoaji wa huduma kwa wateja.
Gavana Kazembe ametoa wito huo
leo jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake iliyolenga kudumisha
uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo.
“Awali kulikuwa na changamoto
kadha wa kadha katika bandari ya Dar es salaam, ambapo kumekuwa na
milolongo mingi wakati wa kupokea mizigo na kutozwa kwa kodi mbalimbali
ikiwemo uhifadhi wa mizigo” alisema Gavana Kazembe.
Alisema kuwa uwepo wa dirisha la
pamoja kwa mteja kuhudumiwa mahitaji yote sehemu moja kumerahisisha
utendaji kazi bandarini hapo na kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara
kutoka nje ya Tanzania.
Aidha, alisema kuwa kwa sasa
mizigo ya DRC inashughulikiwa kwa haraka na hata kodi mbalimbali
zilizokuwa zinatozwa zimepunguzwa, hivyo haoni sababu kwa wananchi wa
DRC kukimbia bandari ya Tanzania.
Kwa upande wake Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Janeth Ruzangi
amesema kuwa, Mamlaka imekamilisha mradi mpya wa Intergrated Security
System (ISS) wenye CCTV camera 486 zenye uwezo wa kuona kila kitu
kinachoendelea ndani ya bandari.
Janeth alisema kuwa Mamlaka
imeanzisha Ofisi Lubumbashi kwa lengo la kuwasogeza zaidi
wafanyabiashara wa DCR ambapo imerahisisha zaidi mchango na huduma
zitolewazo kwa wateja wao.
No comments :
Post a Comment