Sunday, February 12, 2017

SIMBA YAISHUSHA YANGA KILELENI,YAILAZA PRISONS NA KUTUMA SALAMU JANGWANI


simba day 5
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Simba imewashusha kileleni mahasimu wao wakubwa Yanga baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Juma Luizio alikuwa wa kwanza kuiandika bao Simba mnamo dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri toka kwa beki Janvier Besala Bokungu na kumchambua milnda mlango wa Prisons na dakika ya 28 Mshambuliaji mchachari Ibrahim Ajib alifunga la pili baada ya kupokea pasi toka kwa Laudit Mavugo hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo Simba waliweza kunufaika na mabadiliko hayo kwani dakika ya 67 Mrundi Laudit Mavugo alipigilia msumari wa tatu kwa Prisons kwa krosi safi ya Ibrahim Ajib huku likiwa goli lake la tano na akiendelea kung’ara baada ya kuendelea kufumania nyavu mara mbili mfululizo akianza kule mkoani Ruvuma ambapo Simba walishinda jumla ya magoli 3-0 dhidi ya Majimaji huku yeye akifunga bao moja.
Simba wameweza kulipa kisasi hicho baada ya mzunguko wa kwanza kufungwa jumla ya magoli 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya hadi mwamuzi Alex Mahaggi toka Mwanza anamaliza Mpira Simba wameibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha jumla ya pointi 51 na kuwaacha Yanga wakiwa na pointi 49 na wanatarajia kukutana mnamo Februari 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokongu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali/Mwinyi Kazimoto dk62, James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Pastory Athanas dk74 na Juma Luizio/Shizza Kichuya dk70.
Prisons; Laurian Mpalile, Aaron Kalambo, Salum Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sibiyanka, Kazungu Nchinjayi/Kassim Hamisi dk38, Victor Hangaya/Salum Bosco dk76, Mohammed Samatta na Benjamin Asukile/Meshack Suleiman dk56.

No comments :

Post a Comment