Hapa
ni katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa
ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa
manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuvisambaza katika zanahati na
hospitali zilizopo katika manispaa hiyo.
Vifaa tiba hivyo vimetolewa na
Watanzania waishi nchini Denmark ambapo upatikanaji wa vifaa hivyo
unatokana ushirikiano wa Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi
(CHADEMA) na shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga kuwasiliana Watanzania
waishio nchini Denmark kisha kuleta vifaa hivyo.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la AGPAE John Myola alisema wazo
la kutafuta vifaa tiba lilitolewa na diwani wa kata ya Ngokolo Diwani
Emmanuel Ntobi ambaye anajuana na watanzania waishio nchini Denmark.
“Diwani huyu alitupatia
mawasiliano ya watu hao wanaojulikana Denish Relief Group kisha sisi
kama shiriki tukaandika andiko tukiomba kupewa vifaa tiba kwa ajili ya
kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati na hospitali za manispaa
ya Shinyanga”,alisema Myola.
Myola alitumia fursa hiyo
kuiomba ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa
vifaa tiba hivyo vinatumika kama inavyotakiwa na kuhakikisha vinatunzwa.
Naye Diwani wa kata ya Ngokolo
Emmanuel Ntobi alisema watanzania waishio Denmark wametoa vifaa tiba
hivyo bure kwa ajili ya watanzania huku akiishukuru serikali kuruhusu
vifaa hivyo kuingia nchini bila kulipiwa kodi.
“Hili jambo la kidiplomasia kwa
nchi hizi mbili Tanzaia na Denmark,Denish Relief Group ni kundi la watu
la kwanza kutoa msaada mkubwa nchini,huu ni kama mwanzo tu,wamesema
wataendelea kutoa msaada na wamesema wapo tayari kutujengea zahanati
katika kata hii ya Ngokolo ambayo haina zahanati”,alisema Ntobi.
“Tumepokea vifaa tiba aina
26,vimo vitanda,magodoro,viti vya kisasa vya wagonjwa,mashine ya Utra
sound,mashine ya Incubation na vifaa vingine vingi ambavyo vitatumika
katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya
Shinyanga”,aliongeza Ntobi.
Hata hivyo diwani huyo aliomba vifaa hivyo vitumike vizuri na vitumike kwa wananchi wenye kipato cha hali ya chini.
Alisema pamoja na kutoa vifaa
tiba,pia watanzania hao waishio nchini Denmark wametoa baiskeli kwa watu
wenye ulemavu na nguo kwa makundi ya watu wasiojiweza wakiwemo wazee
wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto kilichopo katika manispaa ya
Shinyanga.
Kwa upande wake mgeni rasmi
katika makabidhiano hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika la AGAPE na diwani wa kata
ya Ngokolo katika kupatikana kwa vifaa hivyo.
“Hili ni tukio kubwa na la
busara sana,limetutia moyo ,nawapongeza sana watanzania waishio Denmark
na wote mliofanikisha kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo vitakuwa msaada
mkubwa kwa wananchi,huu siyo muda wa kufanya siasa,kinachotakiwa ni
kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali itikadi za kichama”,alieleza
Matiro.
“Katika suala la
maendeleo,serikali ipo tayari kushirikiana na shirika,kundi lolote la
watu na hata mtu binafsi,tusitumie majukwaa ya maendeleo kufanya
siasa,nimpongeze diwani wa kata hii kwa ushirikiano aliotuonesha katika
kuwasaidia wananchi”,aliongeza Matiro.
Mwandishi
mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa makabidhiano
hayo ametuletea picha 30 za matukio..Tazama hapa chini
Vifaa tiba vilivyotolewa na
watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za
afya katika zahanati na hospitali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga
Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea
Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
Vitanda vya wagonjwa
Vitanda vikiwa na magodoro yake
Afisa Mtendaji wa kata ya
Ngokolo William Ndila akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria
hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio
nchini Denmark “Denish Relief Group” kutokana na jitihada zilizofanywa
na diwani wa kata hiyo Emmanuel Ntobi na Shirika la AGAPE
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akizungumza katika hafla hiyo
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa
shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akielezea namna vifaa
tiba vilipatikana kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya kwa
wananchi wa manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Ngokolo katika
manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) akizungumza wakati wa
hafla ya kukabidhi vifaa tiba hivyo.Kushoto ni diwani wa viti maalum
Zainab Heri (Chadema).Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Diwani wa kata ya Ngokolo katika
manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) aliwashukuru viongozi wa
serikali kwa kuruhusu vifaa tiba hivyo kuingia nchini bila kodi huku
akiomba serikali kuwapatia eneo kwa ajili ya kujenga zahanati katika
kata hiyo ambayo haina zahanati kutokana na kushindwa kujenga baada ya
kuibuka mgogoro kwenye eneo ambapo kulitakiwa pajenge zahanati
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga Magendi Magenzi ambaye ni afisa utumishi wa manispaa
hiyo,akizungumza katika hafla hiyo ambapo kwa namna ya pekee alimpongeza
diwani wa kata ya Ngokolo kwa jitihada alizofanya katika upatikanaji wa
vifaa tiba hivyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ngokolo John Nangi akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alisema
serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali katika
kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kuendeleza siasa kwenye masuala ya maendeleo
Diwani wa kata ya Ngokolo
Emmanuel Ntobi akimwonesha mkuu wa wilaya vifaa tiba hivyo ikiwemo vifaa
vya kubebea watoto na vifaa vya kufanyia mazoezi
Diwani wa kata ya Ngokolo
Emmanuel Ntobi akiendelea kumwonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga vifaa
tiba,pichani ni meza za kulia chakula na kabati
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akionesha vifaa tiba
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiwa ameshikilia fimbo za watu wasioona
Baada ya kukabidhi baiskeli kwa
ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akishikana mkono na Richard ambaye ni mlemavu wa
viungo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimiana na kijana mwenye ulemavu wa viungo baada ya kumkabidhi baiskeli
Wananchi wenye ulemavu wa viungo wakiwa wamekaa kwenye baiskeli
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro na mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola
wakiwasindikiza wananchi wenye ulemavu wa viungo baada ya kuwapatia
baiskeli hizo.Baiskeli hizo zinaendelea kutolewa kwa wananchi mbalimbali
wenye ulemavu wa viungo
Mashine ya Utra Sound ambayo pia imetolewa na watanzania waishio Denmark
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine mbili Utra Sound kwa
ajili ya akina mama wajawazito na Mashine ya kukuzia watoto njiti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine za kisasa za kutolea huduma za afya
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment