Kaimu Mtendaji Mkuu wa PSPTB Bw.
Godfred Mbanyi akifunga mafunzo ya siku tatu katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya (JKCI) jijini Dar es salaam leo , yaliyokuwa na lengo la
kujenga uwezo kwa watendaji wa taasisi hiyo katika mchakato wa Ununuzi
wa Umma, akifafanua zaidi wakati akifunga mafunzo hayo amewaasa
wataalamu hao wa Ununuzi kuvaa joho la Uzalendo wa nchi ili kulitumikia
vyema taifa na watanzania kwa ujumla
Ametolea mfano kuwa “Unaweza
kutumia vibaya fedha kidogo kama Milioni tatu hivi, lakini fedha hiyo ni
muhumu sana kwa maisha ya wananchi kwani kama ingetumika vizuri huenda
ingeweza kununua vitanda kadhaa kwa ajili ya wazazi kujifungulia kule
kijijini na wananchi wakapata unafuu wa maisha kwa kupungumza matatizo
yanayokabili sekta ya afya, Hivyo ni vyema nawaasa kuwa kila mnapofanya
kazi zenu muwafikirie watanzania kwanza kabla ya kijifikiria ninyi
kwanza.
Akitoa neno la Shukurani Dk.
Tulizo Shemu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema mafunzo hayo
yamekuwa muhimu sana kwao na wamepata uelewa jinsi ya kufanya Ununuzi wa
Umma na wameomba kama itapatikana nafasi nyingine ni muhum kupata
mafunzo zaidi ili kuzidi kuelewa mabadiliko ya sheria ya Ununuzi wa
Umma.
Katika Picha kulia ni Ally
Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma PSPTB na kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed
Janabi.
Bw. Hamis Tika Mwanasheria wa PPAA akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyomalizika leo kwenye Taasisi ya JKCI.
Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma PSPTB akizungmza jambo katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akitoa shukurani zake kwa
PSPTB wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Mratibu Mkuu wa Utafiti na
Ushauri PSPTB Bw. Amos Kazinza na Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Umma
na Masoko Bi. Shamim Mdee wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa mafunzo
hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia wakati wa ufungaji mafunzo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments :
Post a Comment