Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana Micronutrient Initiative
Tanzania iliandaa Kikao cha kimataifa cha uhamasishaji wa Afya na Lishe
kwa vijana kilichoanza februari 1, kimefika tamati leo hii februari 3
katika ukumbi wa kimataifa wa Mwaalimu Julius Nyerere,
Dhamira kuu ya kikao hicho
ilikuwa ni kupitia mwongozo Mpya wa WHO wa kuwapa wasichana Madini
Chuma na vitamini ya Foliki Asidi mara moja kwa wiki ili kupambana na
tatizo la upungufu wa damu kwa kundi hili.
Katika kikao hicho
kilichohudhuriwa na nchi zaidi ya tano zikiwemo Senegal, Kenya,
Ethiopia,Canada,wenyeji Tanzania, taasisi mbali mbali na mashirika
yakimataifa ikiwemo WHO, washiriki wote wamekubaliana kwa pamoja ni
lazima kuboresha Afya na lishe ya kundi hili kwakuwa ni kundi ambalo
limesahaulika kwa kipindi Kirefu katika jamii.
No comments :
Post a Comment