Wananchi
wakimuangalia dereva wa teksi aliyejeruhiwa baada ya gari lake lenye
namba za usajili T 625 AWS kugongana na gari dogo lenye namba usajili T
214 CFX wakati likiingia barabara ya Nyerere likitokea Jengo la
Kibiashara la Quality Centre Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwonekano wa Teksi hiyo namba T 625 baada ya kugongana.
Wananchi wakiangalia ajali hiyo.
Wananchi wakiangalia gari dogo
aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX baada ya kuyagonga magari
namba T 741 DEK na T 596 BCG katika eneo hilo la Mtava.
Askari wa Usalama Barabarani akipima ajali hiyo.
Gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX likiwa eneo la ajali kabla ya kuondolewa.
Na Dotto Mwaibale
DEREVA wa
gari dogo teksi yenye namba za usajili T 625 AWS amenusurika kufa baada
ya gari lake alilokuwa akiliendesha kutoka mjini akielekea Uwanja wa
Ndege kugongana na gari dogo lenye namba T 214 CFX aina ya Corolla
lililokuwa likiingia Barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Biashara la
Quality Centre eneo la Mtava jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wakizungumza na waandishi wa habari eneo la ajali
walisema ajali hiyo ilisababishwa na gari hilo dogo aina ya Corolla
lililokuwa likiingia barabara ya Nyerere bila kuchukua tahadhari.
“Chanzo
cha ajali hii ni gari hilo dogo aina ya corolla ambalo liliingia
barabara ya Nyerere bila ya dereva wake kuchukua tahadhari na kama
dereva wa gari namba T 625 AWS angekuwa katika mwendo wa kawaida madhara
yake yasingekuwa makubwa kiasi hicho” alisema shuhuda aliyejitambulisha
kwa jina la Mlugulu.
Mlugulu
alisema baada ya magari hayo kugongana gari hilo aina ya Corolla
liligeuka na kwenda kuyagonga magari mengine namba T 596 BCG na T 741
DEK yaliyokuwa yamesimama yakisubiri kuingia upande ambao lipo Jengo la
Kibiashara la Quality Centre.
Katika ajali hiyo gari namba T 625 AWS liliacha njia na kuhamia upande wa pili wa barabara ya kutoka Tazara kwenda mjini.
Baada ya
ajali askari wa usalama barabarani walifika na kupima ajali hiyo na
kuchukua maelezo ya madereva wote wanne ambapo magari mawili T 214 CFX
na T 625 AWS yakiondolewa na magari ya kukokota magari mabovu (Breck
Down) na kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang’ombe Temeke jijini Dar es
Salaam kwa hatua zingine za kisheria.
No comments :
Post a Comment