Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa
Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Eng. K Tsuji, anayejenga
barabara ya juu (TAZARA fly over) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi
huo jijini Dar es salaam.
Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo
Mitsui Eng. Mitsui Eng. K Tsuji, (Wa pili kulia) akifafanua jambo kuhusu
ramani ya ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over) kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia)
wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akikagua maendeleo ya
Ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya mafundi
wanaojenga barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya
ujenzi ya Sumitomo Mitsui anayejenga barabara ya juu (Fly over)
ya
Tazara kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kupunguza muda wa ujenzi wa
mradi huo.
Akizungumza katika eneo la ujenzi
huo leo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amepongeza hatua
iliyofikiwa sasa lakini pia amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi
huo ili wananchi waweze kunufaika.
“Hakikisheni badala ya kutumia
miezi 35 kujenga mradi huu, mnatumia miezi pungufu zaidi ili kuwawezesha
wananchi na wadau wengine kunufaika na fursa za mradi huu”, amesisitiza
Waziri Mbarawa.
Aidha, Amewataka wafanyakazi wote
katika mradi huo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa kwa kuwa
Serikali ina mpango mwengine wa kujenga Fly over kama hiyo
itakayowawezesha kupata tena fursa ya ajira.
Hatua hiyo itapelekea kuwezesha
wananchi kunufaika na mradi huo mapema, hivyo kupunguza gharama
wanazozipata kutokana na msongamano wa magari uliopo sasa jijini Dar es
salaam.
Naye, Balozi wa Japan nchini Bw.
Masaharu Yoshida, amemhakikishia Waziri huyo kuwa ujenzi wa mradi huo
utamalizika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo kuondoa
changamoto ya msongamano katika barabara ya Nyerere na Mandela.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Crspinius Ako,
amesema kati ya nguzo 66 zinazohitajika kwenye awamu ya kwanza ya ujenzi
huo, tayari nguzo 43 zimeshasimikwa ardhini, hali itayopelekea ujenzi
huo kwenda kwa kasi.
Mpaka sasa mradi huo uliozinduliwa
tarehe 1 Disemba 2015 umekamilika kwa asilimia 25.3 na zaidi ya
shilingi bilioni 96.5 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi huo
ambao utakamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment