Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akisalimiana namwenyeji
wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Jaji
Richard Kibelabaada ya mwenyeji wake kumpokea wakati
akiwasilimkoaniShinyanya kutoa Elimu ya Mpiga Kura mkoanihumo.Kushoto
niNaibuMsajili wa MahakamaKuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje.
Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa
Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akisamiliana na
Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya ShinyangaBw. Geofrey Ramadhani
Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo kutoa Elimu ya
Mpiga kura.
Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa
Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Josephine Matirowakati
alipomtembeleaofisinikwakemkoanihumo.
Mkurugenzi waHudumaza Kisheria wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawisheakitoa Elimu ya Mpiga
kurakupitia Kituo cha redioFarajaFm cha mkoaniShinyangamwishonimwa wiki
hii.Kuliakwake ni mtangazaji wa redio hiyo FaustinKasala.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria
wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga
kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Old
Shinyangailiyopomanispaaya Shinyanga.
Pichana Hussein Makame, NEC.
……………
Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na
kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa
Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Emmanuel Kawishe
wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya manispaa ya
Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.
Alisema kifungu cha 88 cha Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kuchukua
kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia, kukataa kuirudisha au kubaki
nayo kwa uzembe.
Bw. Kawishe alifafanua kuwa
kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu na kipindi cha uchaguzi,
baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura wengine na kuzizuia
kinyume cha Sheria.
Hata, hivyo alisema kutokana na
kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na kuhudhuria maonesho
mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa kadi hizo na kuahidi
kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.
“Kwa hiyo katika jambo hilo
tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini tunachowaomba ukiandikishwa
tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa;
“Jambo la pili mwananchi usikubali
mtu achukue kadi yako ya mpigia kura na wala usitumie kadi yako ya
mpiga kura kwenye kuchukulia dhamana sehemu yoyote”
“Kwa sababu itakwenda kuchukulia
dhamana alafu utashindwa kwenda kupiga kura unapofika wakati wa kupiga
kura, mwananchi ajue kwamba kupiga kura ni haki yake”
Alisema mtu aliyejiandikisha
asipokwenda kupiga kura anakosa haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka na
badala yake anawaacha wenzako wakuchagulie kiongozi.
“Unaacha kupiga kura alafu baadaye
anakuja kulalamika unasema huyu kiongozi simtaki kumbe kura moja
inatosha kubadilisha matokeo ya eneo zima” alisema.
Hivyo aliwasihi wananchi waendelee
kuzingatia amani katika uchaguzi na kuwashukuru kwa jinsi uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015 na uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22 mwaka huu kwa
jinsi ulivyokuwa na amani na utulivu.
”Kwa kweli Watanzania tutambue
kuwa amani ni yetu sisi sote na sisi ndio tutakaoilinda hiyo amani
tuiweke Tanzania yetu kwanza alafu sisi baadaye” aliwakumbusha
Watanzania.
Akijibu swali la mmoja wa
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bukoba aliyehoji anayepoteza kadi ya
mpiga kura anachukuliwa hatua gani kumuwajibisha, Bw. Kawishe alisema
hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake.
Alifafanua kuwa wale wote
wanaopoteza kadi ya mpiga kura wanatakiwa wafike kwenye kituo cha
uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kujieleza na watapatiwa kadi nyingine.
No comments :
Post a Comment