Monday, February 13, 2017

MTANANGE WA KOMBE LA EMIRATES FA SASA MUBASHARA KWENYE VIFURUSHI VYOTE VYA DStv

EMR
Wateja wote wa DStv kushuhudia michuano hiyo bila gharama ya ziada!

Siku chache tu baada ya joto la michuoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON kukamilika nchini Gabon, washabiki wa kandanda nchini wataendelea na utamu wa kandanda baada ya MultiChoice kutangaza kuwa mechi zote zilizosalia za kombe la Emirates FA  sasa
zitaonekana kwenye vifurushi vyote vya DStv kikiwemo kifurushi cha Bomba cha garama ya shilingi 19,975 tu.!
Kuanzia Jumamosi ya tarehe 18 Februari mpaka tarehe 27 Mei, wateja wote wa DStv wataweza kuitazama michuano hiyo mubashara kupitia runinga zao huku michuano hiyo ikiingia kwenye raundi ya tano. Kombe la FA ni moja ya michuano maarufu sana ya mpira wa miguu inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kote duniani.
“Sisi MultiChoice, tunatambua kuwa wateja wetu ni wanazi wa kandanda. Kwakuwa sasa michuano ya AFCON 2017 imemalizika, tunahakikisha kuwa bado wanaendelea kupata burudani kabambe ya mpira wa miguu bila kujali ni mteja wa kifurushi gani cha DStv. Yaani wateja wote wa DStv, sasa watashuhudia mashindano haya mubashara.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande. “Kuongeza , mechi zote zilizosalia za kombe la FA kwenye vifurushi vyote vya DStv bila shaka kutawfanya wateja wetu kupata burudani hii muhimu bila gharama ya ziada.Amefafanua za”
Amesema washabiki na wateja wa ving’amuzi vya DStv watashuhudia mtifuano huo kupitia chaneli za SS3 (SD/HD), SuperSport Select 2, Maximo 1 (SD/HD). Mechi ya ufunguzi wa raundi ya tano itakuwa ni kati ya Mabingwa mara 12 wa michuano hiyo Manchester United dhidi ya Blackburn Rovers mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.
Kwa maelezo zaidi na ratiba za michuano hii tembelea  www.supersport.com

No comments :

Post a Comment