Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimsikiliza
mtoto Oliva Mushi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya
upimaji wa magonjwa ya Moyo. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na
kupima afya bila malipo Mkoani Dodoma ambapo wananchi wa mkoa huo
walipimwa afya zao bila malipo kwa muda wa siku mbili zoezi
lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima mapigo ya moyo Afisa
Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam aliyefika katika banda la
Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo. JKCI ilishiriki
katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo
iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika
katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408 walihudumiwa katika banda
hilo.
Mtaalamu wa Afya na Mazoezi ya
viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania Waziri Ndonde
akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya
moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umuhimu wa
kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya. Wizara ya
Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya
kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku
mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mtaalamu wa Dawa na Tiba kutoka
Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel akiwafundisha wananchi waliokuwa
wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya vyakula bora wanavyotakiwa kula ili
waepukane na magonjwa yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na
Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi
na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa
wa Dodoma.
Mratibu wa Magonjwa yasiyo ya
kuambukiza kwa watu wazima na magonjwa ya saratani kutoka Wizara ya
Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Sara Maongezi akiwafundisha wananchi
waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina za saratani na umuhimu wa
kupima afya mara kwa mara. Hivi karibuni Wizara hiyo ilizindua kampeni
ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bure kwa muda wa siku
mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Twaha Dofa (aliyeshika
karatasi) akitoka kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya
kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa siku mbili
iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments :
Post a Comment