Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria mwanzo
wa urushaji vipindi maalumu vya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akijiweka tayari kurusha
kipindi maalumu cha kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akiiongea na wananchi
ndani ya gari la matangazo la RADIO TIMES mara baada ya kuzindua vipindi
maalumu vya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
………..
Wizara ya Afya, Idara kuu
Maendeleo ya Jamii leo imezindua wa vipindi maalumu vya Radio ambavyo
vinalenga kuelimisha jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
na watoto hapa nchini.
Vipindi hivi vitakuwa vikirushwa
na Radio maalufu nchini ‘RADIO TIMES 100.5 FM ambayo itashirikiana na
wataalamu wa Wizara kusimamia na kuratibu maandalizi ya uendeshaji wa
vipindi vya elimu na stadi za kuzuia ukatili wa kijinsia katika jamii.
Akaiongea katika sherehe fupi ya
uzinduzi wa vipindi hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara kuu
Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema ubunifu wa vipindi hivi na
Radio Times 100.5 ni sehemu ya mwitikio wa tasnia ya habari katika
kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake
na Watoto ambao ulizinduliwa Desemba, 2016.
Ameongeza kuwa uzinduzi wa vipindi
maalum vya elimu kwa umma ni kielelezo thabiti kwamba RADIO TIMES FM
inadhamira ya dhati ya kusaidia juhudi za Serikali kuimarisha ulinzi na
usalama wa mama na mtoto.
Bi Sihaba aliendelea kusema kuwa
anatambua kuwa REDIO TIMES FM ni chombo binafsi ambacho kimetambua kuwa
kinaowajibu wa kuhakikisha kuwa wanawake na watoto katika nchi yetu
wanafurahia upatikanaji wa haki zao na wanaishi katika mazingira salama.
Pia amewapongeza wanahabari wa
vyombo vyote vinavyoelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu athari za
ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kujadili afua zinazotakiwa
kuchukuliwa katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na madhara
ya ukatili huo.
Aidha ametoa rai kwa vyombo
vingine vya habari kufuata nyayo za Radio Times FM katika kukuza uelewa
wa jamii kuhusu athari za ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu Mkuu huyo ametaja ukatili
kuwa na athari ambazo huwapunguzia uwezo wanawake na watoto katika
kupata haki ya kushiriki shughuli za uzalishaji kwa uhuru na amani huku
akaizitaja takwimu za Jeshi la Polisi kuwa zinaonesha vitendo vya
ubakaji kwa mwaka 2015 vilifikia 3,444 na matukio ya shambulio, kujeruhi
na matusi vilikuwa14,561.
Aidha utafiti wa Idadi ya Watu na
Afya ya mwaka 2010 inaonesha kuwa asilimia 39 ya wanawake wa umri wa
miaka 15 – 49 walifanyiwa ukatili wa shambulio na vilevile Taarifa ya
Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto ya mwaka 2011 ilibainisha kuwa
asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana nchini walifanyiwa
ukatili wa vipigo.
Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa
mtoto 1 kati ya watoto 3 wa kike na mtoto 1 kati ya watoto 7 wa kiume
walifanyiwa ukatili wa kingono. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa watoto
15 kati ya watoto 100 wa kike hapa nchini wamefanyiwa ukeketaji.
Kwa ujumla takwimu hizi zinaonesha
jinsi gani tatizo hili lilivyokubwa katika jamii zetu, hivyo ni wajibu
wa kila mmoja wetu kuchukua hatua thabiti kuzuia ukatili huo aliendelea
kusema
No comments :
Post a Comment