Beki wa kati wa Simba
Mganda, Juuko Murshid kurejea kwenye timu hiyo yamepotea baada ya
kupata dili la kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya Red Star Belgrade
ya nchini Serbia.
Beki huyo, hivi sasa
yupo nchini Uganda baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa ya
Uganda ilipokwenda Gabon kucheza Afcon.
Mganda huyo aliondoka
kwenye timu hiyo na kurejea Uganda, tangu kwenye mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Uganda kinachonolewa
na Mserbia, Milutin Sredojević ‘Micho’.
Kwa mujibu wa taarifa
ambazo imezipata Championi Jumatatu, beki huyo wakati wowote atajiunga
na klabu hiyo ambayo iliwahi kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mtoa taarifa huyo
alisema, uongozi wa Simba umemruhusu beki huyo kujiunga na klabu hiyo
kwa lengo ya kujipatia fedha kutokana na mkataba aliobakiza kumalizika
mwishoni mwa msimu huu.
Aliongeza kuwa,
meneja wa beki huyo hivi sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwishoni kwa
ajili ya kujiunga na Belgrade waliowahi kushika nafasi ya pili kwenye
Kombe la Europa na Super Cup.
“Juuko hatarejea tena
kuichezea Simba kwenye mechi hizi zilizobaki za ligi kuu kama
inavyoelezwa, hiyo ni baada ya ofa nzuri ya Klabu ya Belgrade ya Serbia.
“Uongozi wa Simba
umetoa baraka zote za beki huyo kuondoka ili wapate fedha za usajili,
kwani mchezaji huyo anapouzwa, Simba itafaidika kwa mauzo ya mchezaji,
kwa kuwa bado ana mkataba na Simba.
“Simba wamemruhusu
kuondoka kutokana na muda mchache alioubakiza kwenye mkataba wake ambao
unafikia kikomo mwishoni mwa msimu, hivyo kama Simba wakimuachia
mwishoni mwa msimu hawatafaidika chochote, hivyo wameona wamruhusu
kipindi hiki ili wapate fedha,” alisema mtoa taarifa huyo.
Hata hivyo,
alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans
Poppe, alisema hawana mpango wa kumuachia aondoke na badala yake
ataendelea kuwepo kikosini hapo.
Juuko tangu alipoondoka Simba Novemba, mwaka jana, hajarejea nchini kujiunga na wenzake.
“Juuko bado ni
mchezaji wetu na ataendelea kuwa wetu mpaka pale mkataba wake
utakapomalizika. Kutorejea kwake haraka hilo hata lisiwashtue watu, muda
wowote anaweza kurudi na kuungana na wenzake,” alisema Hans Poppe.
No comments :
Post a Comment