Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw.
Godfred Mbanyi akizungumza na wanafunzi waliofikia Level 5
wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi Ugavi
katika Warsha ya Mafunzo ya siku ya Utafiti iliyondaliwa na Bodi hiyo
ambapo kila mwanafunzi atapangiwa msimamizi wa utafiti wake na baadaye
utafiti wao utapimwa kitaalamu ambapo utawawezesha kuwa wataalamu wa
masuala ya Ununuzi wa Umma baada ya Kupata cheti cha kitaaluma cha
(CPSP)
Bw. Godfred Mbanyi amewataka
wanafunzi hao kuwa wasikivu wakati wa mafunzo hayo, lakini pia amewaasa
kuwa na maadili ya kazi zao, Amesema pamoja na kusoma na kuwa na
vyeti lakini kama hawatakuwa na maadili hawatakuwa na umuhimu wowote kwa
bodi na kwa nchi kwa ujumla.
Mbanyi ameongeza kwamba
“Wakimalizia mitihani yao na kufaulu tutawaapisha kiapo cha maadili na
kiapo hicho tutakitumia mahakamani kama ushahidi endapo hawatafuata
maadili katika kazi zao na kuifedhehesha Bodi ya PSPTB) kwa kufanya
mambo bila kufuata utaratibu wa sheria zinazozimamia Ununuzi wa Umma”.
Amemaliza na kusema kwamba
Wataalamu wa masuala ya Ununuzi wa Umma wanashikilia fedha nyingi za
serikali lakini watambue kwamba fedha hizo ni za watanzania na
wanatakiwa kuzitumia vizuri kwa kufuata utaratibu uliowekwa ili ziwe na
manufaa kwa watanzania wote katika kuondokana na changamoto mbalimbali
zinazokwamisha maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla, warsha hiyo
inafanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar
es salaam
Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw.
Godfred Mbanyi akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na
wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Ununuzi wa Umma iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam,
Kulia ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB na kushoto ni
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka.
Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi
wa Mafunzo PSPTB akizungumza katika warsha hiyo katikati ni Bw. Godfred
Mbanyi Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo
Dk Ikandilo Kushoka.
Bw. Godfred Mbanyi Kaimu
Mkurugenzi wa PSPTB akifafanua jambo katika warsha hiyo kushoto ni
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka na kulia ni Amani Ngonyani
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB.
Baadhi ya washiriki wa Warsha
hiyo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw. Godferd Mbanyi hayupo
pichani wakati alipokuwa akizungumza nao.
Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini
Wakifuatilia warsha hiyo kwa umakini mkubwa.
No comments :
Post a Comment