Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akifunga mafunzo ya wanafunzi waliofikia
Level 5 wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na
Ugavi kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Godfred
Mbanyi katika Warsha ya siku tano ya Mafunzo ya Utafiti iliyondaliwa
na Bodi hiyo, ambapo kila mwanafunzi amepangiwa msimamizi wa utafiti
wake na baadaye utafiti wao utapimwa kitaalaam na utawawezesha kufuzu
katika taaluma ya Ununuzi na Ugavi wa Umma baada ya Kupata cheti cha
kitaaluma cha (CPSP)
Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika
kwenye jengo la Taasisi ya Elimu ya watu wazima jijini Dar es salaam
ambapo wanafunzi hao sasa watakwenda kufanya utafiti wao katika maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akimkabidhi zawadi ya kikombe mmoja wa
wanafunzi Sosera Mokiri aliyeshinda bahati nasibu katika ufungaji wa
mafunzo hayo Katikati Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo
(PSPTB)
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akimkabidhi zawadi ya kikombe mmoja wa
wanafunzi Grace Peter aliyeshinda bahati nasibu katika ufungaji wa
mafunzo hayo, Kulia ni Shamim Mdee Afisa Mwandamizi Mahusiano ya Umma
na Masoko (PSPTB) na katikati ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa
Mafunzo (PSPTB)
Baadhi ya washiriki wa mafunzo
hayo wakipokea vyeti vyao kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye katikati ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa
Mafunzo (PSPTB) na kushoto ni Bi. Shamim Mdee Afisa Mwandamizi
Mahusiano ya Umma na Masoko. PSPTB
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye katikati akiwa katika picha ya pamoja na
washindi wa zawadi hizo kutoka kulia ni Grace Peter , Gastor Masawe na
kushoto ni Sosera Mokiri.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
(PSPTB) Bw. Paul Bilabaye katikati na Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa
Mafunzo (PSPTB) wakifurahia jambo wakati Bi. Shamim Mdee Afisa
Mwandamizi Mahusiano ya Umma na Masoko (PSPTB) alipokua akizungumza na
washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye.
No comments :
Post a Comment