Sunday, February 5, 2017

MEYA WA JIJI LA DAR AWATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KUONGEZA UFAULU KATIKA MASOMO MKOA WA DAR ES SALAAM.



 Mchungaji wa Kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera akiongoza ibada katika kanisa hilo lililoko Kimara jijini Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles kuzumgumza na waumini wa kanisa la ufunuo aliposhiriki ibada ya jumapili leo.
 Mchungaji wa kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera (kushoto) akimtambulisha mgeni rasmi kwa waumini Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles kuzumgumza na waumini wa kanisa la ufunuo na kujumuika kwenye ibada ya jumapili leo.
  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles akizungmza na waumini wa kanisa la Ufunuo  wakati aliposhiriki ibada ya jumapili.
 Waumini wa kanisa la Ufuno wakipiga makofi kumpongeza  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles wakati akizunguza.
 Waumini wa kanisa la ufunuo wakishikishiriki kwenye ibada.
 Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kulia) pamoja na Mchungaji wa kanisa   la Ufunuo, Nabii Paul Bendera
(katikati) wakiwa kwenye ibada ya jumapili.
  Waumini wakiwa kwenye maombi ya ibada ya jumapili .
  Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kushiriki ibada ya jumapili kwenye kanisa la ufunuo lililoko kimara jijini Dar es Salaam.
Mchungaji wa kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
…………………..
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewasihi wazazi kushirikiana  na serikali katika maswala ya elimu ili  kuweza kutatua tatizo la kufeli katiaka shule za Serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo hii wakati akifanaya aliposhiriki ibada katika Kanisa   la Ufunuo linaloogozwa na Nabii Paulo Bendera,  lililopo Kimara Jijini Dar es salaam amesema wazazi wanatakiwa kuchunguza watoto wao katika masomo kwakuwa baadhi ya  watoto wanaaga wanakwenda shule lakini hawafiki hivyo inapelekea watoto kutokufanya vizuri.
”Nawasii wazazi  na walezi waendelee kushirikiana na serikali pamoja na bodi ilikuweza kupunguza matokeo mabaya katika mkoa wetu lakini wazazi wawakataze watoto wao kutumia simu kwa sababu watoto wengi wanatumia simu muda mwingi  kuliko muda wa kusoma”amesema Mwita
Nae  Mchungaji wa kanisa  hilo la Ufunuo Nabii Bendera  ameliombea Taifa amani na kuwahasa  watanzania kushirikiana ili waweze kuwa na maendeleo ya kiuchumi.
” Nawaomba watanzania waandelee kuitunza  amani na kuwaombea viongozi wetu  kwakuwa tusipokuwa na amani na ushirikiano hatutoweza kufikia maendeleo tunayo yaitaji” amesema Bendera

No comments :

Post a Comment