Waziri
Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea
banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global
Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya
uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed
Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep
Arya.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya
uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed
Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep
Arya. Picha na mpiga picha wetu.
………….
Na Mwandishi wetu, Dodoma
KUTOKANA
na Tanzania kujikita kufufua uchumi katika sekta ya viwanda vya kati,
Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameihakikishia Tanzania kuisapoti
kwenye suala la elimu kwa lengo la kuinua uchumi.
Akizungumza
wakati akizindua maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha
Wafanyabiashara, Kilimo na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoani Dodoma kwa
kushirikiana na kampuni ya Global Education Link ya Tanzania juzi
(jana), Balozi Arya alisema kukua kwa kasi uchumi wa India, kulitokana
na kuwapo vyuo vingi vya elimu vyenye vifaa vizuri vya kufunduishia
nchini humo.
“Kiwango
cha elimu kinachotolewa India ni cha hali ya juu kutokana na
upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia, jambo
linalowahakikishia wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kupata kazi kwa
urahisi,” alisema Arya na kuwashauri wanaotaka kusoma nje kuwasiliana na
Global Education Link kwa vile wana ushirikiano wa karibu na ubalozi
huo.
Alisema
suala la utandawazi na mahusiano baina ya nchi hiyo na nyingine katika
kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu, linachangia kuwakutanisha
watu wa aina mbalimbali kupata elimu kutokana na kuwapo na vifaa
vilivyopo.
Balozi
Arya aliwahakikishia washiriki wa maonyesho hayo kuwa upatikanaji wa
vifaa vya kisasa vya kufundishia nchini India, kumesaidia kutolewa kwa
kiwango cha juu cha elimu.
Aidha, alisema baadhi ya mashirika makubwa duniani, viongozi wake walifanikiwa kusoma nchini India na kupata elimu iliyo bora.
Ubalozi
wa India umeanzisha ushirikiano na GEL katika kuwasaidia Watanzania
wanaotaka kusoma nje ya nchi hasa baada ya ubalozi huo kujiridhisha na
namna kampuni hiyo ya uwakala wa vyuo vya nje inavyowafuatilia wanafunzi
wake hata baada ya kuwaunganisha na vyuo vya nje kujua maendeleo yao.
Naye
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio
hilo aliwataka watanzania kujiimarisha katika ujuzi akisema ndio msingi
wa kila kitu.
Baadhi
ya wanufaika wa elimu kupitia Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje,
Global Education Link (GEL), akiwamo Pelagia Mauma, alisema alifanikiwa
kupata elimu bora nchini India kupitia kampuni hiyo kwa gharama iliyo
nafuu zaidi.
“Gharama
za elimu katika vyuo vyua India ni nafuu zaidi, hawa wenzetu
hawaangalii ada bali wanachoangalia ni vipi mtu atafanikisha kupata
elimu iliyo bora,” alisema Mauma.
Afisa
Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Dodoma, Fred Azaria pamoja na kueleza
shughuli za chama chake, alisema wanalenga kupunguza umaskini kwa
wananchi wa mkoa wa Dodoma baada ya kuandaa maonyesho ya vifaa vya shule
na zana za kufundishia kutoka India.
“Nawaomba
Watanzania waweze kutumia fursa iliyopo ya kupata elimu, huku
wakiwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kujipatia elimu nchini India,”
alisema.
Nae
Meneja wa GEL tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo alisema sababu ya
kushirikik maonyesho hayo ni kutoa nafasi kwa Watanzania kuhusiana na
namna gani mtu anaweza kufanya uchaguzi sahihi wa kozi ya pale anapotaka
kusoma nje ya nchi.
“Tumekuwa
mawakala wa vyuo vya nje kwa zaidi ya miaka kumi sasa, wengi wamekuwa
wakipitia kwetu kuunganishwa na vyuo vya nje, tumeona tuje hapa ili
waweze kupata ufahamu zaidi kuhusiana na uchaguzi wa vyuo vya nje na
uchaguzi wa masomo ya kusomea pia,” alisema Hemed.
Hemed
alifafanua kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania katika
uchaguzi wa nini cha kusoma. “Utakuta wengi wanachojua ni udaktari,
lakini kwenye udaktari kuna wa aina nyingi, kuna udaktari wa magonjwa
ufahamu, udaktari wa meno tu, udaktari wa mifupa na kadhalika, kazi yetu
ni kutoa ushauri wa aina hii. Tunafanya hivi ili kukumbushana kwa
sababu kama wengi watakuwa kwenye fani au utaalamu wa aina moja, maana
yake ni kwamba fani nyingine zitakosa wataalam au zitakuwa na wataalam
wachache,” alisema.
Mwisho
1. Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
1. Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
No comments :
Post a Comment