Saturday, February 4, 2017

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAANZA


1
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama ametangaza mbio za kuelekea
Tamasha la Pasaka ambalo linataraji kufanyika April 16 Mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Alex Msama amesema
kuwa Tamasha hilo la kusifu na kuabudu,ambalo ni kubwa nchini kuliko
matamasha yote litakuwa la aina yake katika mwaka huu wa 2017.
Msama amesema kuwa kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu itakuwa ni ”Umoja na
upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu” ,Lengo ikiwa ni kudumisha
amani ndani ya nchi yetu  katika kipindi chote
“Napenda kuchukua fursa hii kuwaambia wapenzi wa muziki wa injili kuwa Msama
Promotion imejipanga vyema kwa mwaka huu kuhakikisha kuwa inawaleta watu
pamoja katika sehemu ambayo walikuwa wanaipenda ya kumtukuza mungu kila
wakati wa pasaka kwa kuimba pamoja katika Tamasha la Pasaka wakiwa na
wanamuziki maharufu wa muziki wa injili nchini”amesema Msama.

Msama ameweka wazi kuwa kutokuwepo kwa Tamasha la Krissmas kumezidi kuongeza
ari ya watu kutaka kushiriki tamasha la Pasaka na kujionea mambo
mbalimbali yanayolijumuisha tamasha hilo ambalo huandaliwa kwa umakini mkubwa.
Msama ametoa wito kwa wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika
Tamasha hili ili kuweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji. 

Amesema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litafanyika katika mikoa mitano ili
kuwapa fursa watu wa mikoani kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili na
kusema kuwa tamasha hilo litaanza katika mkoa wa Dar es Salaaam.

Msama alimaliza kusema kuwa kwa sasa yupo katika hatua za kukamilisha vibali
mbalimba vkiwemo vya Baraza Sanaa nchini (BASATA),yote hiyo ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda katika mstari ulionyooka 

2

No comments :

Post a Comment