Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza mmoja wa washiriki
katika kikao cha kuandaa Kanuni za Local Content. Wengine
katika picha ni wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika
pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na
Taasisi zake na wawakilishi wa kampuni za Wachimbaji wa Mafuta na Gesi
Asilia Nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza mada kuhusu Local Content iliyokuwa
ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Wengine ni
washiriki walio hudhuria kikao hicho mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili kulia) akiendesha kikao cha kujadili Kanuni za Local Content
kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG, Marc Hartog (wa kwanza
Kulia) Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Profesa Sufiani Bukurura (wa tatu kulia), Kaimu Kamishna wa
Nishati na masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (wa nne kulia),
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA),
Modestus Lumato (wa tano kulia) pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka
Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),
Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufiani
Bukurura, wa pili ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa James Ntalikwa na wa tatu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG,
Marc Hartog wakiwa katika kikao hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi
(aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu mada zilizotolewa kwenye kikao cha
kujadili Kanuni za Local Content kwenye Ukumbi wa Wizara ya
Nishati na Madini mjini Dodoma. Wanaofatilia ni Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) pamoja na Wenyeviti
wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika na Viongozi Waandamizi
kutoka Wizarani.
Washiriki wa kikao cha Local Content wakifatilia kikao kilicho jadili Kanuni za Local Content mjini Dodoma.
………….
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wachimbaji wa Mafuta na Gesi
Asilia nchini, Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Wakuu wa Mashirika pamoja na
Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake
ili kujadili Kanuni za Local Content kikao hicho kilifanyika tarehe 11-12 mjini Dodoma.
No comments :
Post a Comment