Saturday, February 11, 2017

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA FORODHA DUNIANI ATEMBELEA TRA


KID1Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya alipotembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali  na kuona maendeleo ya miradi ya   Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
KID2
Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya (kulia) akifurahia zawadi ya kitabu cha historia ya Tanzania ambacho Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alimkabidhi kama ishara ya ukumbusho wa ziara yake nchini Tanzania. Dk. Mikuriya alitembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali  na kuona maendeleo ya miradi ya   Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
KID3Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) alipotembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali  na kuona maendeleo ya miradi ya   Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
KID4
Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya  Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (aliyesimama) akitoa maelezo ya jinsi Mfumo wa Forodha (TANCIS) unavyofanya kazi kwa Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya (aliyeketi katikati). Wengine ni Meneja wa Maendeleo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kutoka Shirika la Forodha Duniani Bw. Patrick  Gyan (kushoto) pamoja na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa Bw. Jocktan  Kyamuhanga (kulia).

No comments :

Post a Comment