Saturday, February 11, 2017

SAMATA AWASHA MOTO LIGI KUU YA UBELGIJI,KRC GENK IKING’ARA UGENINI


SAMUUUU
Mshambuliaji  wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya KRC Genk Mbwana Ally Samatta amerejea uwanjani usiku wa jana na kufunga  bao la pili  na likiwa la saba kwake katika ushindi wa 3-0 dhidi ya  Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliochezwa katika Uwanja wa Stayen, Sint-Truiden, St.-Trond.
Samatta aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu aumie mgongo Februari 1, alifunga bao lake dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo fundi wa Kispaniola, Alejandro
Pozuelo Melero. 
Na Pozuelo alitoa pasi kwa  Samatta kufunga bao la pili, akitoka kufunga bao la kwanza yeye mwenyewe dakika ya 37, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji chipukizi Mbelgiji, Siebe Schrijvers.
Bao la tatu la KRC Genk lilifungwa na Ruslan Malinovskiy dakika ya 45 na kuweza kuwadidimiza wenyeji ambao walipanda Ligi Kuu msimu ujao na kwa matokeo hayo KRC Genk imefikisha jumla ya pointi 41 na kuchupa hadi nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi hiyo huku kinara akiwa bado Club Brugge KV wanaongoza wakiwa na alama 52.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley/Wouters dk82, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Boetius dk62 Trossard/Naranjo dk70, Writers na Samatta.
STVV:Pirard, Mechele, Peeters, Gerkens, Bagayoko/Dussaut dk63, Janssens/Boli dk45, Kotysch, Valdivia, Fernandes, Vetokele na Bolingoli/Ceballos dk45.

No comments :

Post a Comment