Saturday, February 11, 2017

Makamu wa Rais Mama Samia aunga mkono uzinduzi wa kitaifa wa mazoezi ya viungo ya kupambana na magonjwa yasioambukizwa mjini Dodoma leo



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kukabidhi matembezi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi mapema leo
asubuhi mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa
wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini
Dodoma.Pichani kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Mh.Nape Nnauye.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
ashiriki kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa
wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini
Dodoma.Mbali ya Makamu wa Rais kuunga mkono tukio hilo pia walikuwepo
viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo,Mh.Nape Nnauye ,Naibu Spika wa Bunge,Tulia Ackson,Waziri wa
Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba,Naibu waziri wa Afya.Maendeleo ya
Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla na
wengineo sambamba na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.

Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa
Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza mazoezi ya kumuunga mkono
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya
kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma

Wananchi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji wa Dodoma wakishiriki mazoezi mapema leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

No comments :

Post a Comment