Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa asilimia 62 ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar es Salaam una jumla
ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 –
64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara
na ajira viwandani.
Awali Tanzania iliweza kutoa
ajira kwa vijana wengi kupitia viwanda vyake vya nguo vilivyokuwa katika
mikoa mbalimbali kama kile cha Urafiki cha Dar es Salaam na vinginevyo
ambavyo hata hivyo kwa sasa viko hoi kutokana na kuhujumiwa na watendaji
wasio waaminifu.
Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu
katika uchumi wa Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya
aina mbalimbali kufuatana na bidhaa zinazozalishwa.
Katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna
bidhaa za aina mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango
kikubwa na kupelekwa nje ya Mkoa.
Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.
Tanzania haiwezi kubadilika ikiwa
mawazo ya watu hayatabadilika katika ujenzi wa viwanda vidogo nchini
kote na kuondoa mawazo ya kujenga viwanda vikubwa kama vya
wafanyanyabiashara wakubwa, kwa kuwa vinahitaji mtaji mkubwa wakati
ajira zake ni chache.
Ama kwa hakika kila mmoja wetu
anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya Dr. John
Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu ya kuwa na
taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia
kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera
ya Tanzania ya viwanda.
Ni kwasababu hiyo tu, watendaji wake aliowaamini na kuwapa
dhamana, hawana budi kuendelea kuwaza zaidi, kutenda zaidi na
kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja waikamilishe ndoto
hii ya Rais wetu mpendwa. Ushirikiano baina ya Makonda na Azimio Housing Estate kampuni ambayo imekubali kutoa eneo lililopo Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470 litakalotumika kama eneo maalumu mbalo litagawiwa kwa wajasiriamali zaidi ya 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo ni mfano wa kuigwa na kupongezwa kwani hii inaonyesha wazi dhamira ya Mheshimiwa Makonda ya kuwakomboa wajasiriamali wadogo wa jiji la Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengineyo mpango
huo unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo kupata maeneo yao
ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo, kuwaepusha
na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika wa
kuwa na anuani (address) za kudumu.
Kutokana na kauli ya Mheshimiwa
Makonda kuna matumaini kwamba neema inawajia wanadar es salaam ya ajira
na soko la bidhaa zao kutokana na ujio wa viwanda hivyo.
Watu wenye viwanda vidogo wana
changamoto nyingi za maeneo na wengine kulazimika kuweka katika maeneo
ya watu na kusababisha kero kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo
hayo.
Kwa ujumla, ujenzi wa viwanda si
kitu kidogo, unahitaji muda na rasilimali nyingine nyingi kufanikisha
hatua inayotarajiwa na umma.
Ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda, inaelekea kutimia baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuonesha
kwa vitendo dhamira yake ya kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.
Mnyonge mnyongeni haki yake
mpeni. Paul Makonda anastahili pongezi kubwa na za dhati kabisa kwa
mkakati wake wa kujenga Dar es Salaam mpya.
No comments :
Post a Comment