Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji
wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl mara baada ya
wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kuwasili
wilayani humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji cha Darakuta kilichopo wilayani Babati mkoani Manyara
Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda ( wa pili kutoka
kulia) na Thomas Ndazi ( wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na watendaji wa kampuni ya Darakuta mara baada ya kumalizika kwa
ziara katika kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl
(katikati) akionesha moja ya chanzo cha maji kinachotumika katika
kuzalisha umeme.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl
(kushoto) akielezea mitambo ya kuzalisha umeme inavyofanya kazi katika
kituo hicho kwa Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kulia)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl
(katikati) akionesha mfumo wa kuongozea mitambo ya kuzalisha umeme ya
kituo hicho.
…………..
Na Greyson Mwase, Manyara.
Imeelezwa kuwa kampuni ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji (Darakuta Hydro Power Project)
iliyopo Babati mkoani Manyara inatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme
kutoka
Kilowati 370 hadi Megawati 1.3 zitakazoingizwa kwenye Gridi ya
Taifa na kupunguza upungufu wa umeme nchini ifikapo mwaka 2021.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo, Raphael Bapsl wilayani Babati mkoani Manyara
wakati wa ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini katika wilaya hiyo, yenye lengo la kuangalia maendeleo
ya miradi ya uzalishaji umeme na kubaini changamoto zake.
Akielezea historia ya mradi huo,
Bapsl alisema kampuni yake ilianza kuzalisha umeme wa Kilowati 50 mwaka
1995 na kuongeza kuwa Aprili mwaka 2016 kampuni ilianza kuliuzia
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umeme unaoingizwa kwenye Gridi ya
Taifa.
Alisema mbali na umeme huo
kutumika kwa matumizi ya nyumbani ambao ni kidogo hususan katika
shughuli za kilimo na ufugaji ili kujiongezea kipato, kampuni yake huuza
umeme wa ziada kwa TANESCO ili kuongeza kiasi cha umeme katika wilaya
ya Babati.
Alisisitiza kuwa ili Tanzania
kuingia katika uchumi wa kati kupitia uwekezaji kwenye viwanda, nishati
ya umeme wa uhakika inahitajika na kuendelea kusema kuwa kwa kutambua
hilo kampuni yake imeweka mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili
kuhakikisha inachangia katika ongezeko la umeme katika Gridi ya Taifa.
No comments :
Post a Comment