DIWANI wa
kata ya Magomeni ,wilayani Bagamoyo,Mwanaharusi Jarhuf,akimnadi mgombea
wa kitongoji cha Magomeni B,Rajab Swedy katika mkutano wa kampeni
uliofanyika eneo la Bagabest.
Meneja wa
kampeni wa uchaguzi mdogo kitongoji cha Magomeni B,Kata ya
Nianjema,Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif,akiwa amepokea kadi kutoka kwa
wanachama wa CUF walioamua kurejea CCM,katika mkutano wa kampeni
ulifanyika Kidongo Chekundu-Bagabest ambapo wanachama Zaidi ya 30 kutoka
CUF walirejea CCM.(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
Mwinyi)
………..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MGOMBEA wa nafasi ya mwenyekiti wa
kitongoji cha Magomeni B,wilayani Bagamoyo, kupitia CCM,Rajabu Swedy
ameahidi kusimamia kero ya ukosefu wa umeme,maji na miundombinu ya
barabara katika maeneo yenye changamoto hiyo.
Amesema endapo atapewa ridhaa na
wananchi siku ya februari 19 mwaka huu,atahakikisha anavalia njuga suala
zima la maendeleo kwa kushirikiana na serikali na wananchi.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiwe Poa,Bagabest na Chemchem Kidongo Chekundu.
Swedy alisema anatambua kero mbalimbali sugu zinazowasumbua wananchi hao hivyo atajituma kwa ari na mali kuzitatua.
Alisema hagombei nafasi hiyo kwa sifa ama maslahi binafsi bali ni kuleta maendeleo ili kupiga hatua kutoka walipo sasa.
“Malengo yangu ni kukabili
changamoto zilizopo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na masuala ya
miundombinu, mikopo,maji,nishati ya umeme, afya na elimu ambayo atayapa
kipaumbele katika kuyapeleka halmashauri”
“Tutakwenda kwa vipaumbele kama
nyie mtakavyo pendekeza kwani lazima tuwe na malengo ya utatuzi wa
changamoto hizi ” alisema Swedy.
Kwa upande wake meneja wa kampeni
ya uchaguzi mdogo kitongoji cha Magomeni B,alhaj Abdul Sharif,alipokea
kadi zaidi ya 30 kutoka kwa wanachama wa CUF ambao wamerejea CCM.
Alisema wanachama hao kurudi CCM inaashiria uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika februari 19 CCM kushinda kwa kishindo.
Sharif aliwaomba wananchi wamchague Swedy na kuachana na wapinzani kwani CCM inatekeleza kwa yale inayoyaahidi.
Sharif alisema Swedy anajiuza kwa
sera na ilani ya chama chake na jimbo la Bagamoyo kuwa na madiwani wote
wa CCM ,hivyo atasaidia kuungana pamoja nao kutatua kero hizo kirahisi.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo Ally Ally Issa,alisema halamshauri hiyo imetenga kiasi cha sh.mil 50 kwa ajili ya kujenga miundombinu kwenye kata ya Nianjema.
Mwenyekiti huyo amabe pia ni
diwani wa kata ya Fukayose ,alifafanua kwamba,fedha hizo zinafikia na
kitongoji cha Magomeni B kujenga na kuboresha miundombinu yake ya
barabara mbovu.
Ally aliwataka wana Magomeni
B,kuacha kufanya makosa ,kuchagua vyama vya upinzani,wasibet katika
uchaguzi huo,bali wamchague RAjabu Swedy
No comments :
Post a Comment