Na.Mwandishi Wetu
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na
muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda
cha kutengeneza vigae “Tiles” katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani
Pwani.
Waziri Mwijage, amesema hayo
alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa
kiwanda hicho cha kutengeneza vigae “Tiles” kitakachotoa ajira kwa
watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne
zisizo rasmi.
“kiwanda hiki kikikamilika
kitasidia sio tu kutoa ajira lakini pia kitasidia kwa watanzania kununua
na kuuza bidhaa zinazotengenezwa nyumani na sio kuangiza kila kitu
kutoa nje”alisema Mwijage.
Waziri Mwijage aliongeza kuwa,”
bidhaa hizi pia zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi,
DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na
kusafirishwa nje ya bara.
Aidha Waziri Mwijage alisema kuwa
kiwanda hicho kitumike vizuri na kutoa wito kwa watanzania kutumia
fursa zitakazo patikana katika mradi huo zitumike kwa faida ya kila
mmoja, “Serikali ya kijiji itambue maeneo yake ili kusaidia kuharakisha
maendeleo ya eneo hili ambapo kiwanda kinafanya shughuli zake”alisema
Mwijage.
Kwa upande Mbunge wa Jimbo la
Chalinze Ridhiwani Kikwete, alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho kipo
katika hatua ya mwanzo ya Ujenzi na kinataraji kukamilika Mwezi wa Saba
na kufunguliwa Rasmi mwezi wa Nane mwaka huu.
Ridhiwani alisema kuwa kiwanda
hicho kitasaidia kufungua mji wa Chalinze na kufanya mji wa viwanda na
biashara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kupanua mji huo,katika
sekta ya viawanda inayosimamia vyema na serikali ya awamu ya tano.
“ujenzi wa kiwanda hiki ni Alama
Chanya ya jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyojidhatiti kufungua fursa
za viwanda katika Nchi yetu.Wananchi wa Chalinze na Pwani wameaswa
kuendelea kujipanga kwa viwanda na fursa nyingi zaidi.”alisema ridhiwani
Ridhiwani aliongeza kwa kunshukuru
muwekezaji huyo pia kwa kukubali kusaidia kumalizia ujenzi wa shule ya
sekondari ya kata ya Pera na kituo cha afya katika kata hiyo.
“licha ya kukubali kusaidia
ujenzi wa huo lakini pia fursa nyingine watu watapata nafasi ya kuuza
mali ghafi zinazotumika kutengeza vigae hivyo ambapo tunatarajia
asilimia 90 malighafi hizo zitatoka hapa kwetu katika mikoa ya
jirani”.alisema Ridhiwani.
No comments :
Post a Comment