Sunday, January 22, 2017

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI



WQA
 Rais wa  Uturuki,  Mheshimiwa  , Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 21, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WQQQ
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 21, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
.
Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 – DAR ES SALAAM
JUMAPILI, JANUARI 22, 2016.

No comments :

Post a Comment