Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Athnony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja naKatibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi Beng’i na watendaji wengine mara baada ya kikoa hicho.
…………………………………………………………………………………………………………
*Waziri Mkuu Kuzindua Feb; Mtaka Ataka Viwanda
*Dk Jingu Asisitiza ubia kwenye ranchi……………………………………………………………
RAS Sagini: nusu ya wakazi wa Itilima ni waganga; Ataka uzalishaji
KUTOKANA na riba kubwa na masharti magumu ya ukopaji katika mabenki ya biashara, wafanyabiashara wadogo wadogo wa Simiyu, wataunganishwa na wafanyabiashara wakubwa duniani ili kupata mitaji na masoko nje ya nchi.
Akitoa taarifa ya Baraza kwa Kamati, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng’I Mazana Issa, alisema Baraza lake tayari limeshaanza kutekeleza mikakati ya kuunganisha mkoa wa Simiyu na wawekezaji ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanashiriki katika shughuli za uwekezaji (local content).
Alisema Baraza lake pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) chini ya mradi wa ‘Tanzania Venture Capital & Private Sector Equity’, watanzindua program ya kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo, wawekezaji wa ndani na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa duniani.
“Wafanyabiashara wadogo wa Simiyu pamoja na wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania, wataingia ubia na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa duniani kupitia utaratibu wa venture capital,” alisema Ms Issa.
Katibu Mtendaji huyo alisema katika utaratibu huo, badala ya wafanyabiashara wadogo kutoka Simiyu na wale wa mikoa mingine kutafuta mikopo yenye riba kubwa na masharti magumu kwenye mabenki “wataingine mikataba na makampuni yenye mitaji na ujuzi kwa makubaliano ambayo pande zote zitanufaika,” alisema mtaalamu huyo wa mambo ya fedha, mitaji na uwekezaji.
Alisema program hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi ujao (4/2/2017) mjini Dodoma na kuongeza kuwa uzinduzi huo utafanywa na Waziri Mkuu, Mh Majaliwa Kassim Majaliwa.
DR JINGU ASHAURI KUHUSU RANCHI
Wakati huo huo mkoa wa simiyu umeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha ranchi binafsi ambazo zitafanya kazi kwa ubia na ranchi za Srikali zilizopo ili kuweka msukumo katika maendeleo ya mifugo nchini.
Akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Simiyu mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dk John Jingu, alisema watu binafsi na hata Halmashauri wanaweza wakaanzisha ranchi ambazo zitaingia ubia na ranchi za serikali.
Tanzania ina ranchi kadhaa za Serikali na zingine za binafsi ikiwa ni pamoja na Ruvu, Mkata, Manyara, Mkwaja, Ndarakwai. Ranchi za Serikali zinamilikiwa na Kampuni ya Ranchi ya Taifa, NARCO.
Dk Jingu aliupongea mkoa wa Simiyu kwa kuwa mfano hai kupigiwa katika shughuli za kuhamasisha uwezesha kiuchumi kwa vile maendeleo ya viwanda ambayo yameanza kukita mizizi katika mkoa huo mpya ni mfano hai unaoonesha kuwa kila kitu kinawezekana tukiamua.
“Kinachotakiwa ni mtaji, masoko na teknolojia ili tuweze kujenga uchumi wa wananchi wetu na hatimaye uchumi wa Taifa zima, Simiyu mmeonesha mfano mzuri wa kuigwa,” alisema.
Alitoa wito kwa viwanda vinavyoanzishwa na kwa wafanyabiashara wote wa Tanzania kuzingatia ubora wa bidhaa akikumbushia mchele wa Tanzania ambao haukununuliwa Dubai tofauti na ule wa Pakistani na India kwa kuwa na mchanganyiko maalum.”
Dk Jingu alihimiza ubora na ‘grading’ ya bidhaa ikiwa ni pamoja na kujua historia ya bidhaa zetu kwa kila tunachozilisha hadi zinapelekwa sokoni ili mteja apate maelezo yote husika huku viwango vya ubora wa kimataifa ukizingatiwa.
No comments :
Post a Comment