Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema
Nchimbi katikati akiwa na Mbunge wa viti maalum Martha Mlata na mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakifanya mazoezi ya viungo katika
uwanja wa shule ya Sekondari baada ya jorging.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akifanya mazoezi na mbunge wa viti maalum Martha Mlata.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.
Rehema Nchimbi katikati akiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu
wakiwa na mshindi wa kwanza wa mbio za Mumbai Marathon Alphonce Simbu
wakifanya mazoezi baada ya kumpokea.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akicheza muziki baada ya mazoezi na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikungi.
Mkuu wa mkoa wa Singida Rehema
Nchimbi akiongoza viongozi na wananchi wa mkoa huo katika uzinduzi wa
mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Hassan
Suluhu la kufanya mazoezi ili kuondoa maradhi yasiyoambukiza na kujenga
mwili
.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu akiruka juu ikiwa ni moja ya mazoezi huku baadhi ya viongozi
akiwemo mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi na mbunge wa viti
maalum Martha Mlata wakimuangalia
…………….
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema
Nchimbi amezindua mazoezi kimkoa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ili kuondoa
maradhi yasiyoambukizwa na kuimarisha afya za wananchi.
Mbali na uzinduzi huo pia
amempokea shujaa mwanariadha Alphonce Simbu ambaye ni mshindi wa kwanza
mbio za Mumbai marathon zilizofanyika mapema mwezi huu huko India.
Akizindua mazoezi hayo leo
wilayani Ikungi mkoani humo, Dk. Nchimbi aempongeza Simbu kwa
kuwakilisha vizuri katika riadha nje ya nje na kuwahamasisha vijana
kuchamkia fursa hiyo ya riadha kwa kuwa inalipa.
“Singida ni tajiri wa mambo mengi
kikubwa tuamue tu,inawezekana kabisa Singida kutoa vipaji zaidi kama
tukijipanga,vijana tumieni fursa hii kwani riadha inalipa na inainua
uchumi kama ilivyotokea kwa Simbu,”alisema dokta Nchimbi.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya
Ikungi Miraji Mtaturu amemuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa wilaya hiyo
imejipanga kuboresha mchezo wa riadha ili kuibua vipaji zaidi vya vijana
na kuendeleza sifa ya wilaya na mkoa kwa ujumla katika kutoa wanariadha
mahiri watakaoiwakilisha Tanzania kama alivyofanya Simbu.
Ameagiza mazoezi kufanyika
jumapili ya pili ya kila mwezi ili kujenga miili yetu na kumpatia Simbu
vifaa vya michezo na ahadi ya shilingo milioni moja kwa ajili ya
kumsaidia kujiandaa na mashindano yajayo
Akitoa shukrani kwa mapokezi Simbu
ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Mampando,kata ya Ntuntu katika wilaya
ya Ikungi amesema mapokezi hayo yamekuwa chachu kwake ya kufanya vizuri
zaidi kwenye mashindano yajayo.
Akisoma taarifa ya chama cha
riadha mkoa katibu wa chama hicho mwalimu Beno Msanga ameshukuru
serikali ya mkoa na wilaya kwa ushirikiano wanaoutoa kusaidia mchezo
wa riadha na kusema kwa sasa wana kambi ya wachezaji 15 kujiandaa
kwenda mashindano ya mbio za nyika mjini Moshi tarehe 17 february 2017.
Aidha amesema kwa kutambua mchango
wa mkuu wa wilaya hiyo Mtaturu chama cha riadha mkoa kimemteua kuwa
mlezi wa Chama hicho mkoa wa Singida.
No comments :
Post a Comment