Sunday, January 29, 2017

RAIS MAGUFULI ATEKELEZA KWA VITENDO MSIMAMO WAKE NA SERIKALI ANAYOIONGOZA WA KUBANA MATUMIZI NA KUOKOA PESA ZA UMMA KATIKA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA


eth1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dr. Augustine Mahiga mara baada ya kuteremka katika ndege ya Ethiopian Airlines iliyomsafirisha kutoka Dar es Salaam hadi jijini Addis Ababa – Ethiopia.

Rais Magufuli alisafiri na ndege ya shirika la Ethiopian Airlines badala ya ndege yake (ndege ya Rais ya serikali) ili kupunguza gharama, kubana matumizi na kuokoa pesa za Umma kwa kupunguza matumizi katika masuala yasiyo na ulazima ikiwemo baadhi ya matumizi katika safari zake za ndani na nje ya nchi.
Rais Dr. Magufuli yupo nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 28 wa viongozi wa mataifa yanayounda Umoja wa Afrika.
Rais wangu… mzalendo na chachu ya matumizi makini ya fedha za Umma katika mambo chanyA+ pekee.

No comments :

Post a Comment