Mwanaharakati
wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald
Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa
Biashara akiwa kwenye mahafali ya 30 ya Chuo cha Africa Graduate
University yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
Askofu
Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches,
akielezea kazi mbalimbali alizofanya kabla ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Waliotunukiwa tuzo wakiwa na furaha katika picha ya pamoja.
Wageni
waalikwa wakiwa na Mama Askofu Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy
(mwenye kofia), alikuwepo kushuhudia mume wake akitunukiwa tuzo hiyo.
Meneja Programu na mshereheshaji katika mahafali hayo,
Lucy Wilson akiwa kazini.
Watunukiwa tuzo hao wakiingia ukumbuni.
Wimbo
wa Taifa ukiimbwa.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa
Ilala, Salum Hamdun ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Stiven Nzowa na kulia ni mke wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe.
Mama Askofu Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy akiomba kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Mkaguzi wa Polisi (ASP) Ezekiel Kyogo akionesha moja ya kitabu alichokiandika chenye manufaa kwa jamii. Kyogo alitunukiwa PhD.
Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha Margaret Mutaleba, akieleza kazi alizozifanya katika jamii.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wasanii wa Bendi ya Jordan wakitumbuiza katika mahafali hayo.
Mwanahabari Tumaini Msowoya, akieleza kazi alizoziandika ambapo zimekifanya chuo hicho kumtunuku Tuzo hiyo ya Heshima.
Watoa huduma katika mahafali hayo, wakiwa katika picha ya [pamoja na Meneja Programu, Lucy Wilson.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa
Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya
Heshima ya Udaktari (PhD), Askofu Dk. Godfrey Mallasy katika mahafali
hayo.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha, Margaret Mutaleba.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Godwin Maimu.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Donald Kisanga.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Mwanahabari
Tumaini Msowoya.
Furaha na tabasamu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Watunukiwa
tuzo hizo, Dk.Donald Kisanga (kushoto) na Mkaguzi wa Polisi (ASP),
Ezekiel Kyogo (kulia), wakiwa na jamaa zao baada ya kutunukiwa tuzo
hiyo.
Viongozi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Dk.Godwin Maimu (kushoto) na Dk.Donald Kisanga wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
CHUO
cha Africa Graduate University cha jijini Dar es Salaam kimewatunuku
Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na watumishi wa mungu
nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada
ya Uzamili HDD.
Watumishi
waliotunukiwa tuzo hizo za heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa
kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa
kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akizungumza
katika mahafali ya 30 ya chuo hicho chenye makao makuu yake Sierra
Leone, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Stiven Nzowa alisema kila mwaka chuo
hicho kimekuwa kikitoa Tuzo za heshima na Shahada za Uzamili kwa
watanzania waliotoa mchango wa kusaidia jamii katika shughuli
mbalimbali.
“Tunao
watunuku tuzo hizi tuzo za heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60
ambao wanafanya kazi za kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya
miaka 15 na kuendelea na wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na
wenye shahada” alisema Profesa Nzowa.
Wakizungumzia
kazi walizozifanya katika jamii Askofu Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la
Tanzania Fellowship of Churches alisema amefanyakazi nyingi za kijamii
ikiwemo kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima na
kubwa zaidi kwa kipindi cha miaka 20 amekuwa akifanya mkesha mkubwa wa
kuliombea taifa amani na yeye akiwa ni mhasisi.
“Kazi
hii ya kuliombea taifa amani tulianza mwaka 1997 na tumeweza kupeleka
huduma hiyo hadi Zanzibar ambako kumefanyika maombi hayo kwa miaka saba
na kuifanya Tanzania kuwa na amani” alisema Dk. Mallasy.
Mwanaharakati
wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald
Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa
Biashara alisema amefanya kazi nyingi za kijamii ikiwa pamoja na
kuishawishi serikali kukagua fedha zinazotolewa na wahisani kwenye
taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kuwatunza watoto yatima baada
ya kubaini baadhi yake zimekuwa zikifuja fedha bila ya kuwasaidia
walengwa.
Mwingine
aliyetunukiwa tuzo hiyo ya heshima ni Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha
Margaret Mutaleba ambaye pamoja na kufanya shughuli nyingi za kijamii
pia ndiye aliyemshauri Rais Dk. John Magufuli kuhusu mpango wa kufanya
usafi ambao unaendelea kutekelezwa nchini kote.
Mbali
na watu hao kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima yupo mwanahabari mahiri wa
gazeti la Mwananchi, Tumaini Msowoya ambaye ametunukiwa PhD kutokana na
kufanya kazi mbalimbali za kijamii kupitia kalamu yake ambazo zimeleta
mrejesho mkubwa kwa walengwa na kuweza kusaidiwa.
Waliotunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari ni Donald Kisanga, Mlute Nyasa, John Pallangyo, Wilson Nyiti na Godwin Maimu.
Wengine
ni Askofu Dk. Godfrey Mallasy, Ofisa wa Jeshi la Polisi Ezekiel Kyogo,
Mtakwimu Margaret Mutaleba na Mwanahabari Tumaini Msowoya.
No comments :
Post a Comment