Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja
katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE)
lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini
Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa
mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na
Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa
nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius
Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda
Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha
Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa
Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia. PICHA NA
IKULU
No comments :
Post a Comment