Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akiwa pamoja na
Mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe, Bw. Juma Irando (katikati), na
maafisa kadhaa wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda,
Biashara naUwekezaji, wakitoka katika Ofisi za Mkurugenzi wa Mji wa
Tunduma kuelekea mpakani mwa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma na
Nakonde
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (aliyeshika mkoba), Mkuu wa
Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Bw. Juma Irando (aliyeshika mikono yake),
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf
Mkenda (Aliyesimama nyuma ya Mkuu wa wilaya), wakisikiliza maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania-Tunduma, Bw. Magori Cosmas (wa pili kulia), kuhusu maandalizi
ya kuanzisha rasmi Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde katika
nchi za Tanzania na Zambia
Afisa Mifumo ya Kompyuta wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw. Yasin Kilima (aliyeshika simu
katikati), akitoa ufafanuzi wa namna TRA ilivyojiandaa kuweka mifumo
itakayo saidia kurahisisha kazi ya utoaji huduma wa pamoja na wenzao wa
Zambia, mbele ya Ujumbe ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia laiyevaa
miwani), wakati walipotembelea mpaka wa Tanzania na Zambia kujionea
maandalizi ya kuanzishwa rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani
unaotarajiwa kuanza Februari mosi, 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akisisitiza jambo
wakati timu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na wizara yake
walipotembelea na kukagua miundombinu ya Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha
Mpakani cha Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, mkoani
Songwe, Bw. Juma Irando, akiongea jambo wakati timu kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
ilipofanya ziara katika Kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde kuangalia
maandalizi ya uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja na Mpakani baada ya
kusainiwa kwa mikataba kati ya Tanzania na Zambia, na kutakiwa kuanza
rasmi mwanzoni mwa Februari, 2017
Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa
Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee (kulia), akiueleza
ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara
na Uwekezaji namna idara yake ilivyojiandaa kuanza kutoa huduma ya
pamoja mpakani kati ya maofisa kutoka Zambia na Tanzania ambao watakuwa
wakitumia ofisi moja kuwahudumia watu wanaotumia mpaka huo kuvuka kwenda
kila upande wa nchi (Tanzania na Zambia)
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa
pamoja na maofisa wa mamlaka ya Mapato kutoka Zambia wakiangalia hali ya
biashara na uwekezaji katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde ikiwa ni
maandalizi ya kuanza rasmi kwa utoaji wa huduma wa pamoja kati ya nchi
hizo mbili ili kuboresha mazingira ya biashara baada ya kusainiwa kwa
mikataba ya kuanzishwa kwa huduma hiyo katika mpaka huo
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa
pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato kutoka Zambia (ZRA)
walipotembelea upande wa pili wa mpaka huo-Nakonde ili kujionea
maandalizi ya kuanza rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya
Tanzania na Zambia baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzishwa kwa
huduma hiyo Februari mosi, 2017
Kituo cha Forodha cha Nakonde Upande wa Zambia
Meneja wa Mamlaka ya Mapato
Zambia-Nakonde, Bw. Nase Lungu, (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo
namna ofisi yake ilivyojipanga kuhudumia wateja wao kupitia utaratibu
mpya wa kushirikiana kwenye jengo moja kati ya maafisa wa Forodha wa
Tanzania na Zambia, wakati Ujumbe kutoka nchi hizo mbili walipotembelea
mpaka huo kujionea maandalizi yalipofikia kabla ya kuanza rasmi kwa
utaratibu huo Februari Mosi, 2017
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (katikati), akisalimiana na
mmoja wa madereva wanaoendesha malori kwenda Zambia, kabla ya kusikiliza
kero zao mbalimbali, ambapo malalamiko makubwa yalikuwa ni kutumia muda
mrefu mpakani mwa Tunduma/Nakonde kunakowatia hasara na kuchelewesha
biashara
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia), akitoa
maelekezo namna ambavyo maofisa wa TRA Tanzania na Zambia wanavyopaswa
kushughulikia kero za madereva na wananchi wanaotumia mpaka wa Tanzania
na Zambia (Tunduma na Nakonde) ili kuboresha biashara mpakani hapo
Ujumbe wa Tanzania na maafisa wa
Zambia walipotembelea na kukagua miundombinu ya utoaji huduma pamoja
baada ya kutiwa saini kwa mikataba ya kuanza kwa Kituo cha Pamoja cha
Mpakani, (Tunduma/Nakonde), huduma inayotarajiwa kuanza rasmi Februari
Mosi, 2017
Ujenzi wa Kituo cha Pamoja Mpakani
upande wa Tanzania-Tunduma, ukiendelea kwa kasi na una tarajiwa
kukamilika baada ya miezi 16 ijayo
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
………….
Na Benny Mwaipaja, WFM, Songwe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amewaonya mawakala wa forodha katika
mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma/Nakonde kuacha Mara moja tabia ya
kuwachelewesha madereva wa malori yaendayo masafa marefu kwa makusudi
ili wapewe rushwa.
Prof. Mkenda ametoa
onyo hilo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, baada ya kupokea
malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva wa malori waliodai wamekuwa
wakicheleweshwa kuvuka mpaka huo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano.
Wadereva hao wameeleza
kuwa mawakala wa forodha wamekuwa wakiwaambia kuwa nyaraka zao
zinazohusika na mizigo wanayosafirisha zimekuwa zilicheleshwa na kituo
cha Forodha upande wa Zambia.
Hata hivyo Meneja wa
Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Kituo cha Nakonde, Bw. Nase Lungu,
amekana kuhusika na ucheleweshaji huo na baada ya ukaguzi wa moja ya
nyaraka hizo ilibainika kuwa upande wa Zambia unatoa nyaraka hizo kwa
wakati lakini zimekuwa zikifichwa na Mawakala wa Forodha upande wa
Tanzania.
Wakitoa ufafanuzi wa
tuhuma hizo, madereva hao wamesema kuwa mawakala wa forodha kwa muda
mrefu wamekuwa wakiwaeleza kuwa mtandao wa intaneti wa Upande wa Zambia
unaotumika kuchakata nyaraka zao uko chini, hivyo walitakiwa kutoa
shilingi 10,000 kwa kila nyaraka ili “kurahisisha” kazi hiyo kwa kuwapa
kitu kidogo maafisa wa forodha wa Zambia.
“Mawakala wengine wa
forodha wana nyumba zao za kulala wageni hapa Tunduma kumbe
wanatulazimisha kukaa hapa ili tulale kwenye nyumba hizo hali inayotutia
hasara na wanatumia kutokujua kwetu kutudanganya kwamba mtandao uko
chini wakijua hatuna uwezo wa kufuatilia huko Zambia” alieleza kwa
masikitiko dereva mmoja
Baada ya kubaini uwepo
wa vitendo hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA
upande wa Tunduma kuandika kibao chenye namba za simu za Mkuu wa TRA
mpakani hapo zitakazotumiwa na madereva wanaocheleweshwa kwa makusudi
kutoa malalamiko yao.
“Tunataka madereva
mtumie siku moja tu kukamilisha nyaraka zenu ili muendelee na safari
yenu vinginevyo tutadumaza biashara kati ya Zambia na Tanzania na pia
tutaifanya Bandari yetu ya Dar es salaam kushindwa kuleta tija”
aliongeza Prof. Mkenda
Alisema kuwa wakala wa
forodha atakayebainika kufanya mchezo huo mchafu wa kuwarubuni madereva
na kuwachelewesha kupeleka mizigo nchini Zambia, watanyang’anywa leseni
zao za biashara.
Meneja Msaidizi wa
Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, mikoa ya Songwe na Mbeya, Bw.
Jomimassa Nsindo, amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na madereva
kukomesha vitendo hivyo ambavyo amesema vinaharibu uchumi na biashara
mpakani hapo.
Naye Mkuu wa wilaya ya
Momba, mkoani Songwe, Bw. Juma Irando, alisema kuwa ataitisha kikao cha
Madereva, Mawakala wa Forodha na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika
Mpaka huo wa Tunduma/Nakonde mapema, ili kuweka msimamo wa serikali na
kuwaeleza wahusika wanaokiuka taratibu hatua watakazochukuliwa.
Prof. Mkenda na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban,
walikwenda katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, kuangalia maandalizi
ya uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya Tanzania na
Zambia, unaotarajiwa kuanza Februari mosi, 2017, baada ya kusainiwa kwa
mikataba kati ya nchi hizo mbili, juzi.
Mwish
No comments :
Post a Comment