Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe. Jaji Memistocles Kaijage akizungumza na wandishi wa Habari
kuhusu upigaji kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani
Zanzibar pamoja na Kata 19 za Udiwani Tanzania Bara utakaofanyika
Januari 22/2017. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Rahaleo Mjini
Zanzibar.
Muandishi wa habari Rahma
Suleiman akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.
Jaji Memistocles katika mkutano wake na wandishi wahabari uliofanyika
katika ukumbi wa Rahaleo.
Mkurugenzi wa huduma za sheria
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emanuel Kawishe akitoa ufafanuzi wa maswali
yaliyoulizwa na wandishi wa habari katika Mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari
walioshiriki mkutano wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
uliofanyika Ukumbi wa Rahaleo Mjini Zanzibar wakifuatilia mkutano huo.
Picha na Makame Mshenga Maelezo.
No comments :
Post a Comment