Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT
Kaangaye kutoka Nyakato Jijini Mwanza, leo wamefanyika Baraka kubwa
baada ya kuhudumu vyema katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma
ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.
Waumini wengi wa Kanisa la EAGT Lumala
Mpya wamefurahishwa na huduma ya kwaya hiyo. Pongezi kubwa ziwaendee
Mwenyekiti wa kwanya hiyo, Abednego Magesa na Mchungaji Samson Mniko kwa
malezi mema yaliyofanikisha wanakwaya hao kumtumikia Mungu kwa bidii
kubwa.
Na Binagi Media Group
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT
Kaangaye lililopo Nyakato Jijini Mwanza, wakihudumu kwa bashasha kubwa
kwenye ibada za hii leo jumapili katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya
lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo kwenye ibada za
hii leo jumapili. Ibada ya kwanza kila jumapili huanza saa 12:00
asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30
asubuhi.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya
lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakimsikiliza
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya
lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia
ibada za leo jumapli
Mahubiri na
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya pia
yanarushwa kupitia runinga ya Star Religion inayopatikana kwenye
kisimbuzi cha Continental ambapo visimbuzi hivyo vinapatikana kanisani
hapo kwa punguzo kubwa.
Picha na Craty Cleophace @EAGT Lumala Mya
No comments :
Post a Comment