Mwenyekti wa Klabu ya Golf ya
Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Brigedia Jenerali
Michael Luwongo akizungumza na Wachezaji wa Klabu hiyo Jijini Dar es
Salaam,wachezaji hao wanataraji Kuwakilisha katika mashindano ya Miaka
10 ya Klabu yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February mwaka huu.(Picha na
Luteni Selemani Semunyu).
Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Brigedia jenerali
Michael Luwongo akisisitiza jambo wakati akizungumza na Baadhi ya
Watendaji wa klabu hiyo hawapo pichani kuhusu maandalizi ya Miaka 10
ya Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani
Semunyu) .
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na
wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa
Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazoezi kwa Ajili ya Maandalizi ya
mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa
kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha
na Luteni Selemani Semunyu) .
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na
wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa
Tanzania ya Lugalo wakijadiliana wakati wa mazoezi kwa ajili ya
mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa
kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha
na Luteni Selemani Semunyu) .
………………
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.
Klabu ya Golf ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo iko katika maandalizi
ya viwanja kwa ajili ya mashindano ya kuadhimisha miaka 10 tangu
kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 2006.
Akizungumza
na waandishi wa Habari msimamizi wa viwanja ambaye pia ni mchezaji wa
kulipwa wa klabu ya Lugalo David Helela alisema kila kitu kinaenda sawa
na wanaangalia sehemu ngumu kuchezeka kuondoa vikwazo visivyo na sababu.
“kuna vikwazo vinavyopaswa kuwepo katika Uwanja wa golf lakini
kuna vikwazo vingine vinakuwepo lakini havina sababu wala havina
mchango katika kuonyesha umahiri wa mchezaji hivyo tunaviondoa”, Alisema
Helela.
Aliongeza
kuwa mbali na kuviondoa bado viwanja kama namba 12 vitaendel;ea kuwa
moja ya kiwanja kigumu kwa mchezaji atakayecheza katika uwanja huo
kutoka na jinsi ulivyowekwa kwa lengo tu la kukamilisha sifa za uwanja
wa Golf.
Helela
Alisema katika kuelekea kuadhimiasha Miaka 10 klabu ya lugalo itabaki
kuwa ndio klabu pekee inayothamini kwa kiwango kikubwa mchango wa
wachezaji wa kulipwa ambao mbali na kuwatumia katika kufundisha vijana
na kusimamia sheria za mchezo lakini wamekuwa wakishirikishwa katika mashindano ya wachezaji wa kulipwa .
Kwa
Upande wake Afisa Tawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule
alisema amefanya ukaguzi wa Awali kazi zinaenda vizuri na kutoa wito kwa
wadhamini kuongeza nguvu ili kuwa na mashindano Bora.
“
Kuna wadhamini tuliofanikia na wako tayari na wameanza maandalizi
lakini Milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kwani
Mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanatarajiwa kuwa ya Aina yake
ukilinganisha na mashindano yaliyowahi kuandaliwa”Alisema kapteni
Mandengule.
Aliongeza
kuwa taarifa rasmi ya mashindano na Mgeni rasmi inatarajiwa kutolewa
hivi karibuni na Mwenyekiti wa Klabu Brigedia Jenerali Michael Luwongo
ili kuelezea kwa kina mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katikati
ya Mwezi wa Pili.
No comments :
Post a Comment