Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Mkuu wa Jeshi la
Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida (kulia) wakati
alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji thamani za ndani na sabuni
katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya
kikazi.
Mkuu wa Kiwanda cha Gereza la
Ruanda ASP Michael Kuga, akisoma taarifa ya hali ya uzalishaji wa sabuni
na thamani za ndani mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa
shughuli za maendeleo zinazofanyika katika magereza yaliyopo jijini
Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akipata maelezo
juu ya utengenezwaji wa kiti kinachotengenezwa na wafungwa wa gereza la
Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Naibu Waziri
yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kulia waliokaa),
akiangalia picha za thamani za ndani zinazotengenezwa na wafungwa wa
Gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la
Magereza.Wengine waliokaa baada ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Kiwanda
hicho,ASP Michael Kuga ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya
Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara
ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza alipotembelea
Kiwanda cha sabuni zinazotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda
wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wanaomsikiliza ni Mkuu
wa Kiwanda() na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya Kamishna
Msaidizi Paul Kajida.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiangalia moja ya
sabuni zinazozalishwa na wafungwa wa Gereza la Luanda wakishirikiana na
wataalamu wa Jeshi la Magereza.Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho.Naibu
Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments :
Post a Comment