Sunday, January 22, 2017

SAMATTA AFUNGA GOLI KRC GENK IKING’ARA UGENINI


SEETTTT
Mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe ambaye ni Nahodha wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk bao la ushindi dhidi ya wenyeji p Eupen katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha basi safi ya Ruslan Malinovysky.
Samatta ambaye amecheza kwa dakika zote 90, alionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Eupen.
Kama si juhudi za kipa wa Eupen Hendrik van Crombrugge, Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars angeweza kufunga mabao mengine.
Kwa ushindi huo Genk imesogea hadi katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 31, huku Club Brugge ikiendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiwa na pointi 43.

No comments :

Post a Comment