Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP)Mzee Nyamka akitoa taarifa
ya utendaji katika mkoa wake kwa Kaimu Kamishna Magereza Dr. Juma Malewa
(hayupo pichani) mwishoni mwa juma hili alipofanya ziara ya kiutendaji
katika baadhi ya Magereza mkoani humo.
Baadhi ya Maafisa na askari wa
Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro wakifuatilia ufafanuzi wa hoja mbalimbali
walizozitoa mbele ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma
Malewa (hayupo pichani) alipofanya ziara kituoni hapo na kufanya Baraza
la watumishi hao ili kusikiliza kero, hoja na mapendekezo yote ikiwa ni
kuboresha utendaji kazi wa siku kwa siku.
Baadhi ya Maafisa na askari wa
Gereza Wami Kuu pamoja na Wami Vijana Mkoani Morogoro kwa pamoja kwa
makini wakifuatilia ufafanuzi wa hoja mbalimbali walizozitoa kwa Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) katika
Baraza la pamoja alipowatembelea hivi karibuni kuona utendaji kazi
katika vituo vyao lakini pia kuwapa hamasa ya utendaji kazi.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kulia) akitembelea jengo la Karakana
ya Ufundi ya Gereza Wami Vijana. Jengo hilo pamoja na kuendelea
kutumika lakini bado linahitaji kukamilishwa kujengwa na kuwekewa
miundombinu ili liweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akipata maelezo mafupi ya kiutendaji
kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu wa Magereza (SP) Zephania
Neligwa (aliyesimama) ofisini kwake wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna
Jenerali Mkoani Morogoro aliyoifanya mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akitolea ufafanuzi hoja
mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya Maafisa na Askari katika kikao
kilichojumuisha askari wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro na
Gereza Mahabusu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati)akisisitiza jambo wakati wa kikao
kikao chake kilichojumuisha askari wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Morogoro na Gereza Mahabusu. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee R.Nyamka. Na kulia
Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa
Magereza (ACP) Joel Bukuku na nawa mwisho ni Mkuu wa Kitengo cha
Uwekezaji na Ujasiliamari wa Jeshi la Magereza Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza (SSP) Uswege Mwakahesya.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa
Gereza Kihonda mara alipowasili kituoni hapo kujionea shughuli
mbalimbali kituoni hapo sanjari na kuongea na maafisa na askari wa
kituo hicho mwishoni mwa Juma hili.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya jengo
jipya la ofisi ya Mkuu wa Gereza Kihonda. Jengo hilo linashengwa kwa
jitihada za Mkuu wa Gereza hilo kwa kushirikiana na maafisa na askari wa
kituo hicho. Viongozi wengine hapo ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka, Mkuu wa
Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza
(ACP) Joel Bukuku na Mkuu wa Gereza Kihonda Kamishna Msaidizi wa
Magereza Ben Mwansasu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa akiendelea kusikiliza hoja mbalimbali za
maafisa na askari wa Gereza Kihonda wakati wa ziara ya kikazi kituoni
hapo. Aliyesimama ni Mkaguzi Msaidizi wa Magereza (A/Insp) Amani Moses
akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa akisalimiana na baadhi ya maafisa wa gereza
Kihonda mara alipowasili akiwa tayari kufanya kikao na watendaji wa
gereza hilo.
Mmoja wa askari wa gereza Kihonda
akiwa na sura ya bashasha baada ya kupata fursa ya kusalimiana na Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza mara baada ya kikao wakati wa ziara ya
Kaimu Kamishna Jenerali katika baadhi ya vituo mkoani Morogoro ikiwemo
gereza Kihonda, mwishoni wa juma hili.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa akikagua maendeleo ya moja ya nyumba za
zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea katika gereza la Wanawake
Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la
uhaba wa nyumba kituoni hapo. Aliyefuatana naye ni Mkuu wa Gereza la
Wanawake Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Luhembe
aimu Kamishna Jenerali wa Magereza
Dr. Juma Malewa (katikati) akitolea ufafanuzi wa jambo katika kikao
chake na watumishi wa gereza Kihonda alipofanya ziara ya kiutendaji
katika baadhi ya Magereza ya mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa
Magereza mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee
Nyamka na kulia Mkuu wa Gereza la Kihonda, Kamishna Msaidizi wa Magereza
(ACP) Ben Mwansasu.
Baadhi ya Maafisa na askari wa
Kingolwira Complex inayojumuisha Chuo cha Uhunzi na Udereva, Gereza
Mtego wa Simba, Gereza Mkono wa Mara na Gereza la Wanawake Kingolwira
katika kikao cha pamoja na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma
Malewa alipofanya ziara katika vituo hivyo kujionea shughuli mbalimbali
za kila siku.
.Sehemu ya Maafisa na askari
wa vituo vya Bwawani Sekondari (inayomilikiwa na Jeshi la Magereza) na
Gereza Ubena mkoani Pwani wakiwa katika kikao cha pamoja na Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani)
alipofanya ziara vituoni hapo ili kujionea shughuli za vitu hivyo lakini
pia kusiliza shida na maoni ya watumishi katika vituo hivyo jana tarehe
28.01. 2017.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani
(RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Boyd Mwambingu akitolea
ufafanuzi moja ya hoja zilizoibuka katika kikao cha Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa na wafanyakazi wa vituo hivyo
alichofanya mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya maafisa na askari wa gereza Wami Kuu na Vijana alipifanya
ziara ya kikazi vituoni hapo.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Mahabusu Morogoro alipofanya
ziara mkoani humo mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya maafisa na askari wa gereza Kihonda alipofanya ziara ya kikazi
kituoni hapo Ijumaa, 27.01.2017.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya maafisa na askari wa Kingolwira Complex mara baada ya kikao
kilicholenga kusikiliza kero na hoja mbalimbali za watumishi hao, tarehe
28.01.2017.
Picha zote na ASP Deodatus Kazinja, PHQ
………….
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Dr. Juma Malewa katika hali ya kuamsha hari na morali ya
kufanya kazi kwa watendaji wa Jeshi la Magereza amefanya ziara ya kikazi
katika baadhi ya Magereza ya Mkoa wa Morogoro na Pwani mwishoni juma
hili.
Ziara hiyo imejumuisha Magereza ya
Mbigiri, Wami Kuu, Wami Vijna, Mahabusu, Kihonda, Kingolwira Complex
yote ya mkoa wa Morogoro na Shule ya Sekondari Bwawani na gereza Ubena
vya mkoani Pwani.
Kutoka kwa Kaimu Jenerali maafisa
na askari aliwapata taarifa fupi ya Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha
sukari cha gereza Mbigiri Mkoani Morogoro kati ya Jeshi la Magereza na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Alisema uwekezaji huu ni kwa
faida ya Jeshi kama Taasisi hivyo ni vizuri kila askari akalifahamu
hilo.
Katika ziara hiyo pia alipata
wasaa wa kufanya vikao na watendaji ambapo maafsa, askari na watumishi
raia walipata fursa ya kuuliza maswali moja kwa moja kutoka kwa Mtendaji
mkuu wa Jeshi la Magereza ambapo baadhi ya mambo yalipatiwa majibu ya
papo hapo na mengine kupewa ahadi ya kutatuliwa katika siku za usoni
hasa yenye uhusiano na masuala ya kibajeti.
Miongoni mwa masuala yaliyoonekana
kuwa ni tatizo sugu ni pamoja na huduma za maji, usafiri, matibabu kwa
wafungwa na mahabusu, sare za askari, posho mbalimbali kulingana na
stahiki ya kila askari na mambo mengine madogo madogo ambayo yote
kimsingi yanagusia suala la fedha.
Katika vikao hivyo Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alitolea maelekezo baadhi ya mambo
yaliyohitaji kauli ya Makao Makuu ya Jeshi lakini pia aliwahakikishia
kuwa ofisi yake itaendelea kushughulikia kero zote na kusaidia kwa
haraka pale inapohitaji kwa kutegemeana na hali ya fedha kwa wakati huo.
Kaimu Kamishna Jenerali aliwaasa
maafisa askari kuwa waangalifu wanapotumia mitandao ya kijamii hasa kwa
kuzingatia viapo vya utumishi wao.
“Ninyi ni askari wenye viapo vya
utii wa mamlaka zilizopo, jiepusheni na mijadala ya mitandaoni kwani
mingine iko kinyume na maadili ya kazi zetu. Ukipokea ujumbe usiofaa
futa kabisa badala ya kuusambaza” alisisitiza Dr. Malewa
Aidha Dr. Malewa aliwataarifu
watumishi hao adhma yake kuu ya kuona Jeshi linakuwa na hospitali kubwa
nayakisasa ili kuondoa kero na aibu inayowapata askari na familia zao
wanapokuja kutibiwa Jijini Dar es salaam.
Ni dhamira yangu kuona tunaanzisha
ujenzi wa hospitali hivi karibuni ili kuondoka na adha ambayo wote
mnaifahamu, na hospitali hii tutaijenga kwa kutumia vyanzo mbali mbali
ikiwemo na sisi kama askari kujitolea. Naomba mtuunge mkono mara wazo
hili litakapoletwa kwenu” alisisitiza Kaimu Jenerali.
Mwisho aliwataka maafisa na askari kudumisha nidhamu kazini ikiwa ndiyo msingi mkuu wa mafanikio hasa katika kazi za majeshi.
No comments :
Post a Comment