Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mamlaka ya usajili wa
vitambulisho vya Taifa(NIDA) imekamilisha zoezi kwa asilimia 93.3%
kuandikisha na kutoa vitambulisho kwa wafayakazi wa sekta ya umma mkoani
Arusha ambapo jumla ya wafanyakazi 26,992 toka kada mbali mbali
serikalini walitarajiwa
kuandikishwa katika zoezi hili ni 25,278 ndio
wameandikishwa na kupewa vitambulisho huku wengine wakishindwa
kujiandikishwa kutokana na sababu mbalimbali
Akisoma Taarifa hiyo wakati
akipokea vitambulisho hivyo vya watumishi wa serikali mkoani hapa
ofisini kwake Katibu Tawala wa mkoa Huo Richard Kwitega alisema kuwa
changamoto kubwa waliokumbana nayo ni kuchelewa kujitokeza kwa baadhi ya
watumishi ambao walikuwa wakichanganya zoezi hilo na zoezi la kuhakiki
vyetu.
Kwitega alisema kuwa pamoja na
changamoto hiyo bado zoezi hilo halikuweza kuathirika ambapo aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye zoezi
linalotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa
Januari,
Alisema kuwa jumla ya makadirio
ya wananchi wanatarajiwa kuandikishwa kwenye zoezi hilo kwa kuchukuliwa
taarifa zao ni 975,988 ambap kwa siku wanatarajia kuandikiasha watu 50
kwa mwandikishaji moja ili kupunguza misongamano.
Akavitaka vyombo vya
habari,viongozi wa umma, kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu
wa vitambulisho vya taifa ili siku ya kuanza kwa zoezi hilo waweze
kujitokeza kwa wingi nakuweza kutumia fursa hiyo.
Alisema ushirikiano wa serikali
na Nida ndio umeweza kufanikisha zoezi hilo kwa watumishi wa umma ambapo
ambao hawajajiandikisha walitokana na wengine kuwa masomoni na wagonjwa
ambapo kwa sasa watawafata huko walipo ili waweze kuwaandikisha wote.
Nae Afisa usajili wa Nida mkoa wa
Arusha Julieth Raymond Mwacha alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri
na kuwataka wananchi kusubiria zamu yao kwa kutoa taarifa zao sahihi za
kuomba kitambulisho cha taifa kwani zoezi hilo hivi karibu litaingia kwa
wananchi wa mkoa mzima.
Alisema kuwa zoezi hilo
likikamilika litaisaida serikali hata kwenye takwimu zake mbali mbali
kwani taarifa zimewekwa kwenye kanzidatam na kukoa fedha ambazo
zingetumika katika mazoezi mengine ya kitakwimu.
No comments :
Post a Comment