Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake leo.
…………………………………………………….
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza nchini
katika maeneo mbalimbali ikiwemo uvuvi katika bahari,madini, utalii,
ujenzi wa viwanda na miundombinu.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa kutoka nchini
China ambao walikuja hapa nchini kutafuta fursa za uwekezaji.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji hao kuwa
Tanzania ni nchi salama kwa ajili ya kuwekeza kutokana na amani iliyopo
na kwa sasa Serikali inaendelea na mkakati kuondoa vikwanzo
vinavyokwamisha uwekezaji ikiwemo
ukiritimba na rushwa nchini.
ukiritimba na rushwa nchini.
Amesema
Tanzania na China zinamahusiano mazuri na ya muda mrefu hivyo ni muhimu
mahusiano hayo yakaendelea kuimarishwa zaidi kama hatua ya kukuza
biashara kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa
Tanzania na China.
Amesisitiza
muhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanya
Biashara wenye Viwanda na Wakulima nchini (TCCIA) na Chama cha Wafanya
biashara kutoka China kama hatua ya kuimarisha kwa angalia fursa bora za
uwekezaji kati ya China na Tanzania.
Makamu
wa Rais pia ameishukuru nchi ya China kwa kuichangua Tanzania kuwa
miongoni mwanchi Nne za bara la Afrika kwa ajili ya uwekezaji wa
viwanda.
Kwa
upande wao, Watendaji hao wa makampuni makubwa kutoka nchini China
wamesema kwa sasa wapo mbioni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza
vifaa tiba katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam na wameshapewa
ekari 160 kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho.
Watendaji
hao wameiomba serikali ya Tanzania isaidie kuhakikisha pindi mradi huo
utakapoanza kujengwa huduma za msingi ikiwemo umeme na maji zinapatikana
kwa urahisi kwenye eneo hilo
No comments :
Post a Comment