Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla katikati
akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kutoa maagizo kwa Mkemia Mkuu
wa Serikali juu ya kufuatilia vilainishi . Kushoto kwake ni Mkemia Mkuu
wa Serikali Prof. Samwel Manyele na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
wizara ya Afya, Dk. Mohammed Ali .
…………………………………………………………….
Na Ally Daud-MAELEZO-Dar es Salaam.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla
amemuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele kuendelea na
uchunguzi wa kimaabara kwa vilainishi vilivyo sokoni ili kubaini bidhaa
isiyokidhi viwango.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam wake na Dkt. Kigwangalla amesema Ofisi
ya Mkemia Mkuu wa Serikali haina budi kuendeleza uchunguzi wa kimaabara
ili kubaini vilainishi visivyo na viwango na ubora ambavyo vinaendelea
kutumiwa.
“Tunapiga marufuku uuzaji wa
vilainishi vya kupima unaofanyika mtaani na sokoni kwa sababu
vifungashio vya vilainishi hivyo havikidhi ubora” alisema Dkt.
Kigwangalla.
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema
Serikali itaendelea kupiga marufuku kuingizwa kwa vilainishi
vilivyotumika (recycled lubricants) visivyo na ubora na visivyo kidhi
matakwa ya kisheria kwani vinachangia uharibifu wa vyombo vya moto
nchini.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla
amesema kuwa asilimia 50 ya vilainishi vya injini, aina ya petroli
zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi
vya kitaifa.
Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa
Serikali, Prof. Samwel Manyele amesema kuwa amepokea agizo la Naibu
Waziri na amesema kuwa uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za vilainishi
zinazoingizwa nchini unafanyika na kuendelea.
Aidha Prof. Manyele amesema kuwa
mpaka sasa wamesajili kampuni 28 za kuingiza vilainishi nchini na
wameimarisha ukaguzi wa mizigo ya vilainishi katika viwanda, bandari,
bandari kavu, mipaka na viwanja vya ndege.
Kwa mujibu wa Prof. Manyele
amesema kuwa miongoni mwa vilainishi hivyo vinavyoingia nchini ni pamoja
na mafuta ya kulainishia injini ,Diseli na Petroli
No comments :
Post a Comment