Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw.
Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini
maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini
Dar es salaam.
Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi
wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika
mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia)
wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili,
Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi.
Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa
nchini Bw. John Reyels.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao
yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
salaam. Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw.
Egon Konchanke akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akielezea namna ya ushirikiano wa
maendeleo kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani unavyoweza kuwa na tija
kwa pande zote, wakati wa kikao kati yake na Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania, Bw. Egon Konchanke, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa ushirikiano kutoka ubalozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi. Julia Hannig, akifafanua jambo wakati
wa kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Mb) na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia),
Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,
Bw. Egon Kochanke (kulia) baada ya kumalizika kwa kikao kati yao,
kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Ushirikiano kutoka
Ujerumani, Bi. Julia Hannig, nje ya Makao makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango baada ya kumalizika kwa mkutano katika ya ujumbe huo kutoka
Ujerumani ukiongozwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon
Kochanke, Jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Hazina)
No comments :
Post a Comment