Na Mahmoud Ahmad Arusha
MAHAKAMA
ya hakimu mkazi Arusha, Desemba 14 imemwachia huru, Mwenyekiti wa UVCCM
,mkoa wa Arusha, aliyesimamishwa Lengai Thomas Sabaya ,baada ya
upande wa Jamhuri kushindwa kuwasilisha ushahidi dhidi yake kwenye kesi
iliyokuwa ikimukabili.
Uanmuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Gwantwa Mwankuga, baada ya upande wa mashitaka kuridhia kufutwa kwa kesi hiyo.
Haklimu alimwambia mtuhumiwa kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kuwasilisha ushahidi mahakama inakuachia huru.
Hata
hivyo mara baada ya kutoka kizimbani Sabaya,ambae pia ni Diwani wa kata
ya Sambasha, wilayani Arumeru, alikamatwa na jeshi la polisi na
kufunguliwa mashitaka mapya .
Kesi
ya awali mtuhumiwa alikuwa akishitakiwa kwa makosa mawili ambayo ni
kujifanya mtumishi wa Umma na shitaka linguine ni kughushi na kujipatia
kitambulisho cha usalama wa taifa kinyume cha sheria.
Upande
wa jamhuri uliwasilishwa na Grace Medikenga, ambae aliiambia mahakama
hiyo iondolewe kwa sababu hawajajipanga hivyo hawaoni haja ya kuendelea
na kesi hiyo.
Kwa
upande wake wakili wa utetezi Yoyo Asubuhi, akizungumza mara baada ya
kesi hiyo kufutwa, amesema kwa mjibuwa sheria mkurugenzi wa mashitaka
anayo mamlaka ya kumkamata mtu pindi anapoaachuiliwa huru na mahakama na
hivyo kufungua mashitaka mapya.
Desemba 7 mahakama hiyo iliuamuru upande wa jamhuri kuhakikisha Desemba 14 unatoa maelezo ya kesi hiyo vinginevyo itaifuta.
Kwenye
kesi hiyo Jamhuri ilikuwa na mashahidi watatu ambao ni Philip John
Sihaki ,ambae ni meneja wa hotel ya Sky way, mwingine ni Inspekta Rogati
wa jeshi lan polisi kituo kikuu cha Arusha, na shahidi wa tatu ni
Editer Evareen kutoka ofisi ya rais.(rso)
No comments :
Post a Comment