Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, kulia akiwa katika ziara ya
ukaguzi wa Mazingira Keko magulumbasi katika mfereji wa maji taka
mseleleko Jijini Dar es salaam mara baada ya kupata malalamiko kutoka
kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akimsikiliza Mtaalamu wa
Mazingira kutoka NEMC, Jaffar Chimgege katika ziara hiyo ya ukaguzi wa
mazingira jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, akiwa ameongozana na wananchi
wanaoishi maeneo ya Keko Magulumbasi katika ziara ya ukaguzi wa
Mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa mazingira Keko
Jijini Dar es salaam.
…………….
NA EVELYN MKOKOI -DSM
Akiwa katika siku nyingine ya
ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, leo ametembelea katika
Maeneo ya keko Magurumbasi na kujionea namna ambavyo wamiliki wa viwanda
wanavyotiririsha maji katika mfereji maarufu kwa jina la mseleleko.
Baada ya ukaguzi wa mazingira
katika maeneo hayo, Naibu Waziri Mpina amewaasa wawekezaji wenye viwanda
nchini waliojenga juu ya miundombinu ya majitaka kutafuta njia nyingine
ya ujenzi sahihi ya miundombinu ya majitaka kutoka viwandani mwao
kwenda kwenye mfumo wa mamlaka za maji na kuelekeza kuwa iwapo
wataonekana kuziba kwa ujenzi wa majengo yao mitaro mikubwa ya
miundombinu ya maji, sheria itachukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na
kubomoa majengo yao.
Akijibu swali la mwandishi wa
habari wa kituo kimoja cha television hapa nchini, lilihoji kuusika kwa
watumishi wa umma kwa namana moja au nyigine kiujanja ujanja katika
kuruhusu vibali vya ujenzi na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya
majitaka na mazingira kwa ujumla, Mpina alisema kuwa endapo
kutagundulika kuwa na ushiriki wowote wa watumishi wa umma katika suala
hilo sheria pia itachukua mkono wake.
Pamoja na hilo Naibu Waziri Mpina
amewaeleza wenye viwanda wanaoendelea kuchafua mazingira kuwa kutakuwa
na oparesheni kubwa nchini ya ukaguzi wa mazingira itakayohusisha
halmashauri za miji, mamlaka za maji, wamiliki wa mabomba ya maji taka
na wananchi ili kuwajibika kwa pamoja katika kunusuru uharibifu wa
mazingira.
Aidha Ameliagiza Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kuiandikia hati ya zuwio
TANROADS ya mwezi mmoja itayowataka wafumue karavati lao linalopita
chini ya barabara katika eneo la kurasini BP darajani na kuliongeza
ukubwa ili majitaka yaweze kupita kwa nafasi.
Naibu waziri Mpina Pia amewataka
Viongozi wa Manispaa ya Ilala kusimamia kikamilifu usafi wa Mazingira na
kuwataka wananchi wa eneo la keko magurumbasi wanaokaa karibu na
mfereji wa mseleleko kufanya usafi katika mfereji huo na kutooutumia
kama DAMPO.
Kwa upande wake mratibu wa
Mazingirawa kanda ya mashariki kutoka NEMC Bw. Jaffari Chimgege amesema
wao kama Baraza watakaa kwa Pamoja na wawekezaji, wenye makaravati
madogo yanazoshindwa kupitisha majitaka vizuri jijini DSM na kutafuta
suluhisho la kudumu kwani hali hiyo ni hatari hasa katika kipindi cha
mvua, inaweza kusababisha magojwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
No comments :
Post a Comment